Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, March 25, 2015

LOWASSA KIDOGO KIDOGO AANZA KUADHIRIKA. HUU NI USHAHIDI TOSHA WAKUWA DISQUALIFIED NA CCM!!

UDANGANYIFU HUO UNAANZA KABLA HATA HAJACHAGULIWA!
Bado tunangojea ujumbe kutoka Pemba eti nao waenda Monduli - ni uwongo mtupu. Hawa wanaokuenda sio Wapemba!
MAPESA WATUIBIE NA WAJINGA WANATUFANYA!!!
Soma kwanza hapa maneno ya baadhi ya Wazanzibari kuhusu Mhe Lowassa: http://zanzibarnikwetu.blogspot.ca/2015/03/wazanzibari-waja-juu-kama-sio-makongoro.html

OOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Image result for lowassa
Masheikh wa Lowassa feki
UKWELI kuhusu wanaodaiwa kuwa viongozi wa dini ya Kiislamu waliomtembelea Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, mjini Dodoma wiki iliyopita umebainika.
Raia Mwema limeambiwa na vyanzo vyake vya kuaminika kwamba katika watu wanaokadiriwa kufikia 50 waliomtembelea Lowassa ili kumshawishi achukue fomu ya kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, waliokuwa na hadhi ya kuitwa masheikh hawafiki hata watatu.


Kwa mujibu wa imani ya dini ya Kiislamu, neno Sheikh humaanisha mtu mzima, muungwana na kiongozi. Kwa mujibu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Sheikh ni miongoni mwa majina yanayotumika kutofautisha viongozi wa dini hiyo na watu wa kawaida.


Ndiyo sababu hata kiongozi wa Bakwata hufahamika pia kama Sheikh Mkuu wa Tanzania.


Mara baada ya kuibuka kwa habari za Lowassa kufuatwa na ‘Masheikh’ hao, Raia Mwema lilifanya uchunguzi na kubaini ukweli kuhusu viongozi hao waliotangazwa katika tukio hilo.

Ziara hiyo inadaiwa kupangwa na Mbunge wa Urambo Magharibi (CCM), Profesa Juma Kapuya, ambaye anadaiwa kutembelea Bagamoyo kupanga mpango huo wa safari hivi karibuni.

“Mheshimiwa Kapuya alikuja hapa Bagamoyo katika siku za karibuni kwenye tamasha la nyama choma na hapo ndipo alipoanza mipango yake ya kuandaa safari hii ya ‘masheikh’.
“Mtu aliyeshirikiana naye kwa karibu kwenye kazi hiyo ni Kassim Mwinyigogo, ambaye ni mmoja wa viongozi wa CCM hapa Bagamoyo na swahiba wa zamani wa Rais Jakaya Kikwete.
“Hao watu waliokwenda Dodoma si viongozi wa Waislamu wa Bagamoyo. Sheikh wa Bagamoyo ni Abdulkadir Ramiya na hakwenda kwenye hilo tukio na wala hakuwa na taarifa ya safari hiyo.


“Ngoja nikuulize swali moja ndugu yangu. Hivi inawezekanaje kwa viongozi 50 wa eneo kama Bagamoyo waondoke na kwenda mbali kama Dodoma pasipo mkubwa wao (Ramiya) kujua? Hapo ndipo waandishi mlipotakiwa kuanza kuuliza maswali,” alisema mmoja wa viongozi wa CCM Bagamoyo aliyezungumza na gazeti hili kwa masharti ya kutotajwa majina.
Gazeti hili limeambiwa kwamba wakati watu hao walipokwenda Dodoma, kila mmoja inadaiwa alipewa kiasi cha shilingi 100,000 na wakati wanarudi walipewa kiasi cha shilingi 400,000 walipoondoka Dodoma.


“Walipoondoka Bagamoyo walipewa shilingi laki moja kila mmoja na taarifa zilikuwa kwamba wanakwenda Dar es Salaam. Lakini ghafla wakaambiwa safari ni ya kwenda Dodoma na labda ndiyo sababu waliongezwa na kupewa laki nne,” kilidai chanzo hicho.


Mwinyigogo anayetajwa katika taarifa hii ni yule mwanasiasa ambaye aliwahi kuwa kada maarufu wa chama cha NCCR-Mageuzi na akitajwa kuwa mmojawapo wa maswahiba wa kisiasa wa Mbunge wa Vunjo, Augustine Mrema.


Katika picha zilizosambazwa, mmoja wa ‘viongozi’ hao alionekana akimkabidhi Lowassa kiasi cha shilingi 700,000 ukiwa ni mchango wao wa kumsaidia aingie katika kinyang’anyiro hicho.


Hata hivyo, Raia Mwema limeambiwa kwamba aliyemkabidhi Lowassa kiasi hicho cha fedha, Yusuf Surulu, aliwahi kuwa kiongozi wa Bakwata Bagamoyo lakini aliondolewa katika wadhifa huo miaka minne iliyopita kwa sababu ambazo gazeti hili haliwezi kuziweka wazi kwa sasa.
Pia, katika picha ambayo Lowassa anaonekana akipokea fedha hizo, huku akiwa na Kapuya; zaidi ya Surulu pia yuko mzee mwingine, Ally Mtumwa, ambaye naye imeelezwa si kiongozi wa Waislamu.


“Huyu Mzee Mtumwa zamani alikuwa miongoni mwa watu wenye uwezo mkubwa wa kifedha hapa Bagamoyo. Lakini katika miaka ya karibuni amekuwa na hali mbaya kifedha na inawezekana sababu za kifedha ndizo zilizosababisha afunge safari hiyo.


“Ukizungumza na watu wa Lowassa wanasema anachofanya yeye ndicho alichofanya Kikwete wakati akiwania urais mwaka 2015. Lakini, basi atumie maarifa kidogo. Mwenzake alikuwa akiwasiliana kwanza na maofisa usalama wa wilaya au mikoa kujua kama anakutana na watu sahihi.


“Sasa huyu bwana aliwahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania na ni lazima anajuana na maofisa usalama hawa ambao wako wengi tu. Anakubalije kuingizwa mkenge kiasi hiki? Mbona masheikh wa Bagamoyo wanafahamika? Hivi siku hizi ushehe ni kuvaa kanzu, koti na baraghashia?” alihoji mmoja wa masheikh maarufu wa Bagamoyo aliyezungumza na gazeti hili Jumatatu, wiki hii.


Duru za kiuchunguzi za gazeti hili zimebaini katika msafara ule uliokwenda kwa Lowassa, wako watendaji wa Bakwata Bagamoyo waliokwenda lakini walifanya hivyo kwa siri na si masheikh kwa sababu yoyote ile.


Wakati akizungumza nao, Lowassa aliwaambia; “Nyie ni maalumu, mnatoka Bagamoyo na inajulikana kwa historia na ni nyumbani kwa Rais Kikwete. Na mimi nimepata baraka zake na nyie mmemuwakilisha,” alisema Lowassa.


“Niseme kwamba ujumbe umefika, mkikutana naye msikitini pelekeni salamu kwa mheshimiwa Rais. Mwambieni mlikuja Dodoma. Mimi nimesema nitaendeleza pale alipomalizia kama Mwenyezi Mungu atanijalia,” alisema.


Mara baada ya kutembelewa na kundi hilo la Bagamoyo, siku iliyofuata Lowassa alitembelewa na kundi lingine la watu wanaodaiwa kuwa wanafunzi kutoka katika Vyuo Vikuu vitatu mkoani Dodoma.


Jumatatu wiki hii, Lowassa alitembelewa na watu wanaodaiwa kuwa viongozi wa makanisa ya Pentekoste hapa nchini; ingawa taarifa nyingine zinadai kuwa ni wafuasi wa Askofu Josephat Gwajima ambaye anatajwa kuwa mfuasi wa Lowassa. Lowassa alishiriki kuzindua helikopta ya Gwajima miezi kadhaa iliyopita.


Wakati gazeti hili likienda mitamboni, kulikuwa na taarifa kwamba kundi lililokuwa linafuata katika ‘ratiba’ iliyopangwa ni Umoja wa Vijana wa CCM Wilaya ya Bagamoyo. Eneo hilo la Mkoa wa Pwani linatajwa kuwekwa kimkakati kwa vile mpango unatajwa kuwa kuwaaminisha Watanzania kwamba Lowassa anaungwa mkono na Kikwete.


Akizungumza juzi Jumatatu, Lowassa alikana madai ya yeye kutumia fedha kuwahonga watu wanaokwenda nyumbani kwake kumshawishi, akidai kwamba hana uwezo huo kifedha.
“Ninyi mmekuja huku kwa sababu ya mapenzi yenu kwa Mungu wenu na taifa lenu. Wanaodai kwamba mimi ninawapa watu hela ili waje wanaeneza upuuzi tu,” alisema mbunge huyo wa Monduli.


Mwishoni mwa wiki iliyopita, Sheikh Ramiya alizungumza na waandishi wa habari mjini Bagamoyo na kuwaambia kwamba hawatambui viongozi hao waliokwenda Dodoma kwa vile si viongozi wa Waislamu kama ilivyodaiwa na kambi ya Lowassa.


Hatua hiyo ya Lowassa tayari imeanza kuibua maswali miongoni mwa wana CCM ambapo tayari Mbunge wa Bumbuli na Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, January Makamba, amehoji kuhusu ukweli wa ziara hizo za kumuomba mwanasiasa huyo agombee.


Katika toleo lake la juzi Jumatatu, gazeti dada la hili, Raia Tanzania lilimnukuu Makamba akisema; “Urais ni nafasi ya hadhi na heshima kubwa. Unapoiomba hupaswi kufanya michezo ya kuigiza. Huu utaratibu wa kuratibu watu, kuwasafirisha, kuwapa posho na ubwabwa waje kukuomba ugombee ni michezo ya kuigiza ambayo ni aibu kubwa”.


http://www.raiamwema.co.tz/masheikh-wa-lowassa-feki

No comments :

Post a Comment