Hili blog ni kuhusu Tanzania na dunia nzima kwa ujumla. Pita kila siku kwa habari moto moto. (This blog is about Tanzania and the world as a whole. Pass-by everyday for breaking news). ***********************KARIBUNI NYOTE / YOU ARE ALL WELCOME!***********************
Thursday, March 5, 2015
Mahojiano ya Mh Tundu Lissu katika kipindi cha Mkasi
Ingekuwa shule ya msingi, ungemuita Toto Tundu, kwa jinsi mwalimu anavyopata shida kukubaliana nae, ila katika hali aliyopo sasa, si tofauti sana....Namzungumzia Mhe. Tundu Lissu. Mmoja kati ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alie mahiri kwa kusema bila woga, na mwenye sifa ya kusumbua kiti kwa hoja zake makini ila mara nyingi zenye kuchokoza na kuhamsha mijadala motomoto.
Mtaalamu wa Sheria, na mmoja wa Mawakili wenye ruhusa ya kitaaluma kutetea katika mahakama zetu, Mhe Lissu amekuwa mmoja kati ya wabunge walioweza kuweka bayana utata wa kisheria unaoibuka katika hoja mbali mbali ndani ya Bunge, na pia amekuwa mstari wa mbele katika harakati mbalimbali za kisiasa na kijamii hasa pale msaada wa kisheria unapohitajika.
Wanamkasi wameamua kumuita kikaangoni, tuweze kushiriki nanyi yale machache aliyonayo, kadri muda unavyoruhusu.
Salama, Mubah na John ana kwa ana na Mhe Lissu kwenye Mkasi
Yote kwa hisani ya Coca Cola, Tusker Tanzania na Airtel Tanzania.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment