Mshauri wa mikakati wa Katibu Mkuu wa CUF Mansour Yussuf Himid, akiwaonyesha kidole watoto waliovalia sare za CUF (hawapo pichani), baada ya kuwasili katika kisiwa cha Kojani kwa ajili ya kuhutubia mkutano wa hadhara.
Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano ya Umma wa CUF Salim Bimani, akionesha zawadi alizokabidhiwa na wananchi wa Kojani kwenye mkutano wa hadhara wa CUF uliofanyika kiwani humo mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya wanachama, wapenzi wa CUF na wananchi waliojitokeza katika mkutano wa hadhara wa CUF uliofanyika Kojani mwisho mwa wiki.
Watendaji wa CUF Wilaya ya Wete wakionesha kadi na Katiba ya CCM, walizokabidhiwa na wanachama waliokihama chama hicho na kujiunga na CUF kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kojani.
Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano ya Umma wa CUF Salim Bimani, akionesha kadi na katiba ya CCM alizokadhiwa na wanachama waliokihama chama hicho na kujiunga na CUF kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kojani.
Baadhi ya wanachama, wapenzi wa CUF na wananchi waliojitokeza katika mkutano wa hadhara wa CUF uliofanyika Kojani mwisho mwa wiki. (Picha kwa hisani ya CUF).
Chanzo: ZanziNews
No comments :
Post a Comment