Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, March 26, 2015

Tibaijuka, Muhongo kuibukia kwa ‘Zitto?’


Prof Tibaijuka ambae alikuwa mfano bora kwa wanawake wa nchi hii alipoteza heshima yake kwa rushwa ya Escrow. Siku za Nyerere jina lake lingelikuwa linatajwa kila kabla ya taarifa ya habari kutokana na ujingiri huo wa Escrow!


Prof Muhongo nae pia alipoteza heshima yake katika Taifa hili kutokana na shoddy business deals wizarani kwake!

oooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo
WALIOKUWA mawaziri wawili wa Rais Jakaya Kikwete huenda wakawa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ambayo ripoti yake kuhusu akaunti ya Escrow ndiyo iliyosababisha waachie ngazi, Raia Mwema limeambiwa.
Kwa mujibu wa taratibu za Bunge, mawaziri hawatakiwi kuwa wajumbe wa kamati lakini kila mbunge anatakiwa kuwa mjumbe wa mojawapo ya Kamati za Bunge zilizopo ili aweze kutimiza majukumu yake ipasavyo.
Kwa vile Tibaijuka na Muhongo sasa si mawaziri tena, wanapaswa sasa kuingia katika mojawapo ya kamati hizo kama ambavyo Spika wa Bunge, Anne Makinda, ataamua kuwapangia.
Gazeti hili limeambiwa na duru za kibunge mjini Dodoma wiki iliyopita kwamba Profesa Tibaijuka tayari ameandika barua kwa Spika kuomba kupangiwa kamati na “kuna uwezekano akawa ameomba kuwemo kwenye kamati ya PAC”.
“ Nasikia Tibaijuka ameomba awekwe kwenye kamati ya PAC. Hili si tatizo kwa sababu mbunge anaweza kuomba lakini mwenye uamuzi wa mwisho ni Spika ambaye ndiye anayeamua mbunge awekwe kwenye kamati ipi.
“ Hapa tulipo tunasubiri kwa hamu kuona Makinda atampangia kamati ipi Tibaijuka kwa sababu kama kweli ameomba PAC, basi itakuwa patashika huko. Maana ni vigumu kujua lengo lake hasa ni lipi lakini pia itaonyesha ujasiri na ukomavu alionao wa kuweza kufanya kazi na yeyote,” alisema mmoja wa wabunge kutoka Mkoa wa Kagera aliyezungumza kwa masharti ya kutotajwa jina.
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu kutoka jimboni kwake Muleba Kusini juzi Jumatatu, Tibaijuka alisema yeye anasubiri tu kuona amepangiwa kamati gani na Spika na atafanya kazi na kamati yoyote atakayopangiwa.
“Mimi sijaomba kufanya kazi na kamati yoyote. Vyovyote nitakavyopangiwa nitafanya tu kwa sababu mimi ni mwanasiasa mbobezi na nina uzoefu wa kutosha wa shughuli za kibunge na serikali. Hapa nilipo niko jimboni kwangu nachapa kazi na wananchi wangu.
“Kama Spika ataona nitaweza kusaidia kama nitafanya kazi za PAC mimi sitakuwa na shida. Kama ataona ninaweza kusaidia zaidi kama nitafanya kwenye kamati ya ardhi na mazingira, nitafanya tu. Sina tatizo na mbunge wala kamati yoyote,” alisema Tibaijuka.
Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa PAC, Deo Filikunjombe, alisema wao hawana tatizo lolote na Tibaijuka na kwamba watakuwa tayari kufanya naye kazi kama Spika ataona mchango wake unahitajika.
“Si Tibaijuka peke yake. Ikiwezekana wamlete na Profesa Sospeter Muhongo maana naye atakuwa hajapata kamati hadi sasa. Sisi tukiletewa mtu wa kufanya naye kazi tutafanya naye kazi tu bila matatizo,” alisema Filikunjome.
Kamati ya PAC hivi sasa inaongozwa na Mbunge wa Viti Maalumu kutoka Chama cha Wananchi (CUF), Amina Mwidau, akichukua nafasi ya Zitto Kabwe ambaye amejiengua uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na hivyo kupoteza ubunge wake. Hivi sasa yeye ni mwanachama wa chama cha ACT.
Chini ya Zitto, PAC ilichunguza suala la akaunti ya Tegeta Escrow ambalo baadaye lilikuja kusababisha Muhongo, aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema na Tibaijuka kuondoka madarakani kwa sababu tofauti.
Kwa mujibu wa rekodi rasmi za Bunge, Mwidau anakuwa Mwenyekiti wa kwanza mwanamke wa kamati hiyo tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi; huku wengine waliowahi kushika nafasi wakiwa ni Mwenyekiti wa Chama cha United Democratic (UDP) na Mbunge wa Bariadi Magharibi, John Cheyo na Zitto.
Tibaijuka aliponzwa na taarifa kwamba alipokea kiasi cha shilingi bilioni 1.6 kutoka kwa mfanyabiashara James Burchard Rugemalira, ambaye ni mmoja wa waliofaidika kifedha na uuzwaji wenye utata wa kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL).
Kwa upande wake, Muhongo anadaiwa kufanya maamuzi yaliyosababisha serikali ipate hasara katika suala hilo la Escrow, ingawa yeye aliachia ngazi mwenyewe kwa maelezo kuwa hataki kuendelea na malumbano kuhusu jambo hilo.
Werema aliandika mwenyewe barua ya kujiuzulu wadhifa wake huo kwa Rais Kikwete akieleza kwamba ushauri wake kuhusu suala hilo la Tegeta Escrow haukueleweka na umeleta sintofahamu ambayo hangependa iendelee kwa yeye kubaki madarakani.
Kwa kawaida, imekuwa kawaida kwa Makinda kuwapangia mawaziri kamati ambazo zinaendana na wizara walizokuwa, mfano ukiwa wa William Ngeleja ambaye alipoondolewa kwenye Uwaziri wa Wizara ya Nishati na Madini, Spika alimpangia kwenye Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini.
Mawaziri wengine ambao walipelekwa katika wizara walizowahi kuzifanyia kazi ni Profesa Peter Msolla aliyekuwa Wizara ya Kilimo ambaye sasa amepelekwa katika Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira.
Wengine ni Ezekiel Maige aliyepelekwa Nishati na Madini na Shamsi Vuai Nahodha aliyepelekwa Kamati ya Ulinzi na Usalama akitoka kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

No comments :

Post a Comment