Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, March 8, 2015

RAIS WA ZANZIBAR DR MOHAMED SHEIN AFANYA UFUNGUZI WA HOTEL YA HYATT ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akikata utepe kama ishara ya ufunguzi wa Hotel ya Park Hyatt Zanzibar iliyopo Mambo Msiige Mji Mkongwe wa Zanzibar (kulia) Kaimu Waziri wa Fedha na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Makame Mwadini (kushoto) Mmiliki wa Hoteli hiyo Sheikh Ali Sayeed Albawardy.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akifungua pazia kuashiria ufunguzi wa Hotel ya Park Hyatt Zanzibar iliyopo Mambo Msiige Mji Mkongwe wa Zanzibar (kulia) Kaimu Waziri wa Fedha na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Makame Mwadini (katikati) Mmiliki wa Hoteli hiyo Sheikh Ali Sayeed Albawardy.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akifuatana naSheikh Ali Sayeed Albawardy mmiliki wa Hotel ya Park Hyatt Zanzibar alipotembelea sehemu mbali mbali za Hoteli hiyo iliyopo Mambo Msiige Mji Mkongwe wa Zanzibar baada ya kuifungua rasmi leo,
Wasoma utenzi Amina Mohamed na Khadija Ridhiwani (kulia) walipokuwa wakitoa burudani hiyo mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pamoja na viongozi mbali mbali wakati wa sherehe za Ufunguzi wa Hotel ya Park Hyatt Zanzibar iliyopo mtaa wa Mambo Msiige Mji Mkongwe wa Zanzibar leo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Makame Mwadini akiwa Kaimu waziri wa Fedha alipokuwa akitoa hotuba yake ya ufunguzi waHotel ya Park Hyatt Zanzibar kwa wananchi pamoja na kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein azungumze na Wananachi baada ya kuifungua Hoteli hiyo iliyopo mtaa waMambo Msiige Mji Mkongwe wa Zanzibar leo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake wakati alipokuwa akizungumza na wananchi na Viongozi mbali mbali na wawekezaji walioalikwa katika ufunguzi wa Hotel ya Park Hyatt Zanzibar yenye hadhi ya juu katikamtaa wa Mambo Msiige Mji Mkongwe wa Zanzibar leo.

Baadhi ya waalikwa mbali mbali wakiwemo wawekezaji na wafanyabiashara wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na wananchi na Viongozi mbali mbali na wawekezaji walioalikwa katika ufunguzi wa Hotel ya Park Hyatt Zanzibar yenye hadhi ya juu katika mtaa wa Mambo Msiige Mji Mkongwe wa Zanzibar leo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akiagana na Sheikh Ali Sayeed Albawardy baada ya kumalizika kwa sherehe za ufunguzi wa Hotel ya Park Hyatt Zanzibar iliyopo Mambo Msiige Mji Mkongwe wa Zanzibar (katikati) Meneja Mkuu wa Hoteli hiyo Bi Mercela Heeendoerfer.
[Picha na Ikulu.]

No comments :

Post a Comment