Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, March 1, 2015

Shaka amsimanga Maalim Seif kutibiwa nje ya nchi

  • Asema ni ajabu kiongozi wa CUF kwenda kinyume na ahadi zake
Zanzibar. Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana(UVCCM), Shaka Hamdu Shaka amesema uchumi wa Zanzibar ungekuwa mbovu, Serikali isingeweza kumlipia Sh80 milioni kila safari moja, Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad kwenda kutibiwa India.
Shaka alitoa tamko hilo jana katika mkutano uliofanyika kwenye Ofisi Kuu ya UVCCM, Zanzibar.
Image result for shaka of uvccm
Shaka Hamdu Shaka 
Katika mkutano huo na waandishi wa habari, Shaka alitumia muda mwingi kujibu hotuba ya Maalim Seif na viongozi wengine wa Chama cha Wananchi (CUF) iliyohutubiwa kwenye uzinduzi wa Kamati za Ushindi kueleka Uchaguzi Mkuu mwaka huu.
Shaka alisema UVCCM imesikitishwa na kauli ya Maalim Seif akibeza kuwa Seikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) ni ya kidhalimu na haijajenga uchumi imara.
Alisema ni jambo la kushangaza kumuona kiongozi huyo wa CUF akienda kinyume na ahadi zake alizotoa kwa wananchi za kutibiwa nchini, lakini  anaongoza kwa kusafiri za nje ya nchi, kuliko kiongozi mwingine kwa matibabu, huku akitumia kiasi kikubwa cha fedha za umma.
“Tumeshtushwa na matamshi ya Maalim Seif akibeza kuwa uchumi wa Zanzibar umezorota, takwimu zinaonyesha uchumi umekuwa kwa asilimia 7.4 mwaka 2013/14, hakuna mtoto anayetembea zaidi ya kilomita tano kufuata shule au kukosekana kituo cha afya.
“Kuna barabara za lami, vifo vya mama na watoto vimepungua na malaria imebaki historia,” alisema Shaka.
Hata hivyo, aliponda uzinduzi wa kampeni za CUF na kusema ni mbwembwe na mikogo ambayo haiwezi kukisaidia chama hicho kushinda katika Uchaguzi Mkuu na kuingia Ikulu, kwa sababu kina mgombea mmoja wa kudumu, kina viongozi wenye tuhuma za ufisadi na ubadhirifu, hakina uzalendo wala mipango ya kisera.
“Sherehe na mbwembwe siyo vigezo vya kushinda uchaguzi, huwezi kuwa na chama cha siasa chenye mgombea mmoja wa kudumu... hiyo siyo demokrasia ya kweli na hakiwezi kukubalika kitaifa na kimataifa,” alisema.
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Umma CUF, Salum Bimani alisema madai ya Shaka hayana msingi wowote.
Alisisitiza kuwa  hali ya uchumi wa Zanzibar chini ya uongozi wa sera za CCM, ni mbovu, huku akisema wananchi wanakabiliwa na maisha magumu.
Bimani alisema vijana hawana ajira, wamepoteza matumaini, wanashinda vijiweni, huku vigogo wa CCM wakila nchi na kufuja rasilimali...huku  watoto wao wakisoma na kufanya kazi nje ya nchi, wakati viwanda vyote vimekufa na hawaonyeshi kuleta utatuzi.
“Uchaguzi wa mwaka huu CCM itafute mahali pa kutokea, tumewabana mbavu na wananchi hawawataki, hatutakubali kuibiwa kura zetu, ila tukishindwa kihalali tutakubali, lakini kwa kura moja mtu mmoja,” alisema Bimani.

No comments :

Post a Comment