Ndugu wananchi na wafanya biashara, kama mnavyojua kuwa hivi sasa tunakabiliwa na kipindi cha mvua za masika zinazotarajiwa kunyesha hivi karibuni ambapo mvua hizo zinatarajiwa kuwa kubwa kwa mujibu wa taarifa za zinazotolewa na wataalamu wa mamlaka ya hali ya hewa tanzania kanda ya zanzibar.
Kutokana na uzoefu wa mvua za masika maranyingi mji wetu huathiriwa na mafuriko katika mitaa na kusababisha athari kubwa kwa jamii kama vile maradhi ya mripuko(kipindupindu,matumbo ya kuharisha na kuharisha damu,homa ya dengue,uharibifu wa makaazi , upotevu wa mali na hata kusababisha vifo kwa wananchi.
Hivi sasa baadhi ya wananchi wanatabia ya ya kuchafua mazingira na kuhatarisha afya za wakaazi kwa kufanya mambo yafuatayo kinyume na utaratibu na sheria nayo ni:
· utupaji taka ovyo katika maeneo ya makaazi,magofu,maeneo ya wazi na ndani ya michirizi na mitaro ya maji ya mvua.
· uuzaji holela wa biashara za matunda na vyakula kama vile juisi ya maji ya muwa,mamalishe,urojo,chipsi na samaki wa kukaanga katika maeneo machafu na yasiyoruhusiwa kisheria na kutofuata kanuni za afya.
· kutiririsha maji machafu ovyo mitaani ambayo husababishwa na ukosefu na kujaa kwa makaro.
· ukosefu wa vyoo na kufanya haja kubwa ovyo .
· kuwa na makaazi yaliyozungukwa na majani marefu.
Kwa taarifa hii baraza la manispaa linawaomba wananchi,viongozi wa shehia na wadi,wafanyabiashara,vikundi vya mazingira na wadau mbali kufanya mambo yafuatayo:
· kusafisha mazingira yanayokuzunguka kwa kuondoa taka na kufyeka majani marefu mitaani.
· kuzuia umwagaji wa maji machafu ovyo mitaani na kusafisha michirizi ya maji ya mvua
· kufukia vidimbwi vyote vya maji ili kudhibiti mazalio ya mbu nk.
· kutupa taka katika maeneo ya majaa maalum yaliotengwa na manispaa kwa ajili ya kuhifadhia taka hizo.
· kuzuia uuzaji wa vyakula katika mazingira machafu na yasiyoruhusiwa kisheria kama vile juisi ya maji ya miwa, mama lishe, urojo, chipsi nakadhalika.
· kusafisha maeneo yote ya magereji ya magari na magofu yaliotupwa taka kinyume na sheria.
· kuacha tabia ya kutupa taka katika mitaro na michirizi ya maji ya mvua.
· kutouza biashara za vyakula wazi na kutopanga biashara chini hasa katika maeneo ya masoko.
· kuandaa utaratibu wa kusafisha mitaa kwa mashirikiano na vikundi vya usafi vya shehia na wadi.
Katika kukabiliana na changamoto zilizotajwa baraza la manispaa Zanzibar limepanga mikakati ya kuimarisha usafi wa mazingira kwa kushirikisha wafanyakazi wake,vikundi vya usafi,viongozi wa shehia na wadi na wadau mbalimbali kufanya yafuatayo.
· kusafisha na kuweka makontena katika vituo vya taka kwa utaratibu maalum.
· kuimarisha timu ya ukaguzi wa afya na mazingira katika mitaa,maeneo ya biashara na masoko ili kuhakisha kuwa mashart,kanuni na sheria za usafi zinatekelezwa
· kuhamasisha viongozi wa mitaa madiwani na masheha kuandaa mpango wa usafi katika shehia na kuelimisha jamii juu ya matumizi mazuri makontena ya taka yanayotarajiwa kuwekwa hivi karibun.
· kusfisha mitaro ya maji ya mvua kwa kushirikisha vikundi vya kijamii kwa kujitolea na kulinda uhalibifu usitokee.
· kutoa elimu ya usafi na mazingira kupitia vyombo vya habari,mikutano ya jamii mitaani.
· kuendeleza zoezi la operesheni maalumu ya kuzoa na kuondosha taka majaani
· kutanua huduma za usafi katika maeneo yasiyokua na huduma hiyo.
Ili kufanikisha adhima hii baraza la manispaa linawaomba wananchi,wafanyabiashara,viongozi wa mitaa,vikundi vya usafi,kamati za afya na mazingira na wadau mbali mbali kusimamia kikamilifu mpango huu ili kuimamarisha usafi wa mazinira na afya za wananchi na wageni wanaotembelea nchi yetu.
“kinga ni bora kuliko tiba”
No comments :
Post a Comment