Kongamani la Kuitakia Nchi Amani katika Mchakato wa Kura ya Maoni ya Katiba Iliopendekezwa na Uchaguzi Mkuu
Mwenyekiti wa Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini Shekh Noman Thabit Jongo akitowa maelezo ya Kongamano la Amani kuzungumzia Katiba Iliopendekezwa na Bunge Maalum la Katiba Tanzania, Kongamano hilo lililofanyika katika ukumbi wa hoteli ya bwawani Zanzibar na kuwashirikisha Viongozi wa Dini, Mashekh, Maimamu, Viongozi wa Taasisi za Kijamii na Vijana wa Wemawema (walikuwa wakijiita Ubaya ubaya )
Shekh Fatawi Bin Issa Mjumbe wa Baraza la Maulamaa Mkoa wa Kusini Unguja akisoma dua kabla ya kuaza kwa Kongamano hilo la Viongozi wa Dini kuzungumzia Amani katika kipindi cha Kura ya Maoni ya Katiba Mpya iliopendekezwan na Bunge Maalum la Katiba na Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.
Baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo wakiitikia dua.
Mkuu wa Wilaya ya Magharibu Unguja Mhe Ayoub Mohammed akifungua Kongamano la Viongozi wa Dini Zanzibar kuzungumzia Katiba Iliopendekezwa na Bunge Maalum la Katiba Tanzania juu ya Amani kwa Wananchi wakati wa kupiga kura ya maoni, Na kuwataka Viongozi wa Dini wana wajibu mkubwa kutunza amani kutokana na majukumu waliokuwa nayo kwa waumini wao, ndio watunzaji wakuu wa amani.
Washiriki wakifuatilia hutuba ya Mkuu wa Wilaya ya Magharibi wakati wa ufunguzi wa Kongamano hilo.
Washiriki wakifuatilia hutuba ya Mkuu wa Wilaya ya Magharibi wakati wa ufunguzi wa Kongamano hilo.
Washiriki wakifuatilia hutuba ya Mkuu wa Wilaya ya Magharibi wakati wa ufunguzi wa Kongamano hilo.
Mchungaji akichangia Mada katika Kongamano hilo la Amani lililotayarisha na Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini Zanzibar.Na kusema hapa tunazungumzia Amani kwa Tanzania Biblia huzungumzia amani na kutowa wito kwa Viongozi wa dini na kujiepusha na mambo ya siasa na kutokupandikiza katika dini, Kiongozi wa dininanayejihusisha na siasa katika dini kiongozi huyu ni kufukuzwa ndio wanaohatarisha amani kupitia dini.Katiba hii iko sawa kwa kila mtu na dini zote bila ya kupndelea mtu auwatu.
Shekh wa Madrasa Jangombe akichangia mada ya Amani iliowasilishwa na Shekh Noman Jongo.
Wakuu wa Meza Kuu wakifuatilia Mjadala wa kuchangia Mada walizowasilisha katika Kongamano hilo la Viongozi wa Dini Zanzibar katika ukumbi wa hoteli ya bwawani Zanzibar.Mtoa Mada Mhe Hamad Rashid akifuatilia michango hiyo ikiwasdilishwa.
Mchangiaji akitowa Shukrani kwa Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini Zanzibar kwa mada ilizowakilisha kuhusuana na Utunzaji wa Amani kwa Wananchi wa Tanzania, amesema kuna baadhi ya watu hupotosha baadhi ya Ibara za Katiba kwa kutowa nusu nusu na kutafsiri isivyo na kutolea mfano Ibara inayohusu Ardhi hii hupotoshwa sana.
Shekh Mohammed, akichangia katika Kongamani hilo la kuitakia Amani Tanzania katika Uchaguzi Mkuu na Kura ya Maoni, akitowa maoni yake juu ya kudumisha amani kwa kufuati maadili ya dini kuna baadhi ya Wananchi wanakwenda kinyume na mafundisho ya dini na kudiriki kuvunja amaani kwa kukosa mafundisho ya kitabu cha mwenyezi mungu.
Washiriki wa Kongamani la kuzungumzia Katiba Mpya iliopendekezwa na Bunge Maalum la Katiba wakifuatilia michango inayotolewa na Washiriki wa Kongamano hili lililoandaliwa na Kamati ya Amani ya Maridhiano ya dini za Kiislamu na Kikristo lililofanyika ukumbi wa Bwawani hoteli.
Chanzo: ZanziNews
No comments :
Post a Comment