Katika mahojiano maalumu na gazeti hili, Naibu Katibu huyo amewataka wananchi kuipuuza kauli hiyo na kuwahimiza kuisoma Katiba inayopendekezwa ili wakati ukifika wafanye maamuzi sahihi na kutumia haki yao kidemokrasia.
Alisema kuwa Katiba inayopendekezwa ni suluhisho la changamoto na kero za Muungano ambazo zimekuwa zikilalamikiwa kwa muda mrefu na kwamba kutoipigia kura Katiba hiyo ni kuhalalisha kuendelea kutumika kwa katiba iliyopo ambayo ina upungufu.
“Kama hatukuipigia kura katiba hii unafikiri mafuta ambayo tumekuwa tukiyadai tutayapata wapi, mikopo ya nje tutaipata wapi, hapa ni lazima wananchi wapime kuhusu kauli hii,” alisema.
Aidha, aliwataka viongozi wa vyama vya upinzani wanaoipinga Katiba inayopendekezwa kuwapa uhuru wananchi wa kuamua wenyewe kulingana na maoni yao baada ya kuisoma katiba hiyo.
“Hii ni katiba ya watanzania wote na hizi kauli za viongozi akiwamo makamo wa kwanza wa rais ni kama kuwalazimisha wananchi kufuata maoni yake jambo ambalo linapingana na misingi ya utawala bora,” alisema.
Katika hatua nyingine, aliwataka wananchi wa Zanzibar hususani Kisiwani Pemba kuacha kuwa watumwa wa kisiasa kwa kuwaepuka viongozi wanaojali maslahi yao binafsi bali waangalie viongozi wenye nia ya kuwaletea maendeleo.
Alisema kuwa majimbo ya Pemba ambayo vingozi wake, wabunge na wawakilishi ambao wanatoka chama cha CUF wameshindwa kuwaletea mabadiliko ya maendeleo na badala yake waangalie viongozi walio na uwezo wa kuleta maendeleo katika majimbo yao bila ya ubaguzi.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment