Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, March 8, 2015

Zanzibar yahimiza maendeleo ya wanawake



Wakati dunia ikiadhimisha Siku ya Wanawake leo, Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Maendeleo ya Vijana, Wanawake na Watoto Zanzibar, imeitaka jamii na taifa kuleta maendeleo ya wanawake.

Waziri wa wizara hiyo, Zainab Mohammed Omar, katika taarifa yake ya maadhimisho hayo, alisema wanawake wakiendelezwa, kutapatikana familia na taifa lenye uwezo wa kupambana na kuondokana na umasikini.

Alisema kila mmoja ni shahidi wa hatua na jitihada zinazochukuliwa na serikali ya Zanzibar katika kuinua kiwango cha maendeleo na hali ya wanawake nchini, ambazo alisema zimeweza kuleta mabadiliko makubwa.

Alizitaja baadhi ya jitihada hizo kuwa ni kutoa fursa zaidi za elimu kwa wanawake kwa kuwawahamasisha watoto wa kike na wazazi kutoa kipaumbele kwa wanafunzi wa kike kuendelea na elimu badala ya kuozeshwa wakiwa katika umri mdogo.

Alisema jitihada nyingine ni kuwaondolea malipo akina mama wanaojifungulia katika hospitali za serikali, jambo lililowapa faraja wananchi.

Hata hivyo, alisema bado wanawake wa Zanzibar wanakabiliwa na changamoto za ukatili na udhalilishaji wa kijinsia, licha ya kauli ya hivi karibuni ya Rais Dk. Ali Mohamed Shein, kuwataka wananchi wote kushiriki katika mapambao na kupiga vita vitendo hivyo dhidi ya wanawake na watoto.

Kaulimbiu ya mwaka huu kwa Zanzibar ni, “Timiza ahadi, chukua hatua madhubuti katika kunyanyua hali za wanawake Zanzibar”.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

No comments :

Post a Comment