zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, April 12, 2015

Chakula kwa wanakamati mbali mbali za Sherehe za Mapinduzi

Kikundi cha JKU Morden Taarab kiitumbiza wakati wa chakula cha Usiku  kilichoandaliwa rasmi kwa Halmashauri ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa pamoja kamati mbali mbali zilizofanikisha Sherehe hizo hafal ilifanyika jana viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa na Viongozi katika 
chakula cha usiku  kilichoandaliwa rasmi kwa Halmashauri ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa katika kufanikisha Sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar  ya miaka 51  katika viwanja Ikulu Mjini Unguja jana 
Waalikwa walioshiriki katika chakula cha usiku  kilichoandaliwa rasmi kwa Halmashauri ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa katika kufanikisha Sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar  ya miaka 51  katika viwanja Ikulu Mjini Unguja jana
Baadhi ya waalikwa katika  katika chakula cha usiku  kilichoandaliwa rasmi kwa Halmashauri ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa katika kufanikisha Sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar  ya miaka 51  katika viwanja Ikulu Mjini Unguja jana wakifuatilia kwa makini taratibu wakati wa chakula hicho ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
Waalikwa walioshiriki katika chakula cha usiku  kilichoandaliwa rasmi kwa Halmashauri ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa katika kufanikisha Sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar  ya miaka 51  katika viwanja Ikulu Mjini Unguja jana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akichukua chakula wakati wa hafla maalum kwa Halmashauri ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa katika kufanikisha Sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar  ya miaka 51  katika viwanja Ikulu Mjini Unguja jana
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzinbar Balozi Seif Ali Iddi pamoja na Viongozi mbali mbali walishiriki katika 
hafla maalum ya chakula cha usiku kwa Halmashauri ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa katika kufanikisha Sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar  ya miaka 51  katika viwanja Ikulu Mjini Unguja jana
Baadhi ya Viongozi wakichukua chakula katikahafla ya chakula cha Usiku  kilichoandaliwa rasmi kwa Halmashauri ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa pamoja kamati mbali mbali zilizofanikisha Sherehe hizo hafal ilifanyika jana viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar
Baadhi ya waalikwa katika  katika chakula cha usiku  kilichoandaliwa rasmi kwa Halmashauri ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa katika kufanikisha Sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar  ya miaka 51  katika viwanja Ikulu Mjini Unguja jana wakifuatilia kwa makini taratibu wakati wa chakula hicho ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
Baadhi ya waalikwa wakichukua chakula katikahafla ya chakula cha Usiku  kilichoandaliwa rasmi kwa Halmashauri ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa pamoja kamati mbali mbali zilizofanikisha Sherehe hizo hafal ilifanyika jana viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Makame Mwadini akitoa neno la Shukurani kwa Niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein wakati wa hafla ya chakula cha Usiku  kilichoandaliwa rasmi kwa Halmashauri ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa pamoja kamati mbali mbali zilizofanikisha Sherehe za maiaka 51 ya mapinduzi matukufu ya Zanzibar zilizofanyika viwanja vya Ikulu, 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Barza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na Viongozi baada ya kumalizika kwa hafla ya chakula cha usiku  kilichoandaliwa rasmi kwa Halmashauri ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa katika kufanukisha Sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibarya miaka 51  katika viwanja Ikulu Mjini Unguja jana,[Picha na Ikulu.]


Dk.Shein Aishukuru Halmashauri ya Sherehe za Maadhimisho ya Kitaifa kwa Kufanikisha Sherehe za Miaka 51 ya Mapinduzi.

STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
    Zanzibar                                                                                                       12 Aprili, 2015
---
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameiongeza Halmashauri ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa kwa kusimamia vyema maandalizi na kufanikisha maadhimisho ya sherehe za miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Katika hafla fupi ya chakula cha jioni iliyofanyika Ikulu jana kwa ajili ya kuipongeza na kutoa shukrani kwa Halmashauri, Dk. Shein alisema Halmashauri hiyo ilifanya kazi vizuri kwa kushirikiana na kamati zake ndogondogo hadi sherehe hizo kufanyika kwa mafanikio makubwa.
Akizungumza kwa niaba ya Mheshimiwa Rais, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dk. Mwinyihaji Makame alizishukuru Kamati Tendaji za Halmashauri hiyo pamoja na vyombo vya habari na vikundi vya sanaa kwa ushirikiano wao hadi kufanikisha sherehe hizo.
Kamati ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa inaongozwa na Mwenyekiti ambaye ni Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd na Makamu Mwenyekiti wake ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Mheshimiwa Haji Omar Kheir ambao wote walihudhuria hafla hiyo.
Mapema akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mheshimiwa Mohamed Aboud alimshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuandaa hafla hiyo ambayo aliielezea kuwa ni uthibitisho sio tu kuwa Halmashauri hiyo na Kamati Tendaji zake zilifanya wajibu wake ipasavyo na zilistahili pongezi lakini pia ni kielelzo cha imani aliyonayo Mheshimiwa Rais kwa wajumbe wa Halmashauri hiyo na Kamati zake.
Aidha Mheshimiwa Waziri alimshukuru Mheshimiwa Rais kwa kushiriki kikamilifu katika ratiba za shughuli mbalimbali za maadhimisho hayo iliyotolewa na Halmashauri hiyo hadi siku ya kilele chake.
Katika mnasaba huo waziri huyo alimhakikishia Mheshimiwa Rais kuwa Halmashauri hiyo itaendelea kutekeleza wajibu wake kikamilifu katika kufanikisha maadhimisho yajayo.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na wajumbe wa Halmashauri ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa, Kamati Tendaji kumi za Halmashauri hiyo, sekretarieti yake pamoja na vikundi mbalimbali vya Sanaa vilivvoshiriki maadhimisho hayo na waandishi wa habari.   
Postal Address: 2422 Tel.+255 776 613 015, Fax: 024 2231822 

No comments :

Post a Comment