Dk. Shein aliyasema hayo wakati akizungumza na vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kupokea maandamano yao ya kumuenzi Karume, katika ofisi kuu ya CCM Kisiwandui.
Alisema nchi inakabiliwa na uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu, hivyo hatakuwa tayari kuona mtu au kikundi cha watu kuibeza amani ya nchi.
Alisema Karume alikuwa mtu wa watu kutokana na vitendo vyake vikiwamo vya kuhimiza amani kwa vitendo, kuhimiza umoja na mshikamano na kupinga ubaguzi.Aliwataka vijana hao kujituma na kufanya kazi kwa bidii, kuwa waadilifu na kuchukia ubinafsi kwani hivyo ndivyo vitendo vya Rais wa kwanza wa Zanzibar alivyokuwa akivifanya.
“Vijana muwe tayari kuitumikia nchi na kuendeleza Muungano huu wa serikali mbili ambao uliasisiwa na viongozi wetu Mzee Karume na Mwalimu Nyerere,” alisema Dk. Shein.
Aliwasisitiza vijana hao kufuata misingi ya Mzee Karume ikiwamo kuepuka udanganyifu kwa sababu bila ya uwadilifu taifa halitajengeka na maendeleo hayatapatikana.
Aidha, Dk. Shein alisema ipo haja ya kumbukumbu za Mzee Karume kukusanywa na kisha kutolewa elimu mashuleni kuhusu historia yake ili kizazi cha sasa na kijacho kiifahamu.
Vijana hao walikuwa na matembezi ya kumuenzi kiongozi huyo waliyoanzia kijiji cha Mwera Kiongoni alikozaliwa Mzee Karume hadi ofisi kuu ya CCM Kisiwandui alikozikwa.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment