zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, April 8, 2015

Dk. Shein aongoza kumbukumbu ya Karume

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dk. Ali Mohamed Shein, ameongoza mamia ya wananchi kuadhimisha Siku ya Mashujaa wa Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964.
Maadhimisho hayo yalifanyika katika Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui, Zanzibar kisha Rais Shein aliwaongoza wananchi kutembelea kaburi la aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Hayati Abeid Karume.
Wakati wa maadhimisho hayo yaliyoanza jana saa moja asubuhi, walikuwapo mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini, viongozi wa Serikali na wa kidini.
Baadhi ya viongozi waliohudhuria ni pamoja na Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.

Wengine ni Rais mstaafu wa Zanzibar, Aman Abeid Karume, Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Othman Makungu, Katibu Mkuu Kiongozi wa Zanzibar, Abdulhamid Yahya Mzee na Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir Kificho.
Viongozi wa kidini waliokuwapo ni pamoja na Askofu wa Kanisa la Anglikana, Michael Henry Hafidh, Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Saleh Omar Kabhi, Kadhi Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Khamis Haji Khamis na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salim.
Akizungumza na MTANZANIA kuhusu maadhimisho hayo, mwasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar, Hamid Ameir, alisema viongozi waliopo madarakani wanatakiwa kufanya kazi kwa kufuata maadili ya kazi kama alivyofanya hayati Karume.
Naye mke wa hayati Karume, Fatma Karume, aliwataka Watanzania wadumishe amani kwa kuwa ndilo jambo alilokuwa akilisisitiza hayati Karume.
“Pia Serikali iwe makini na kuwachukulia hatua za kisheria wanasiasa wanaoeneza siasa za kuwabagua Wazanzibari na wanaoishi Tanzania Bara,” alisema.


http://mtanzania.co.tz/?p=3483

No comments :

Post a Comment