Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Othman Makungu, jana aliwaapisha wasuluhishi na waamuzi watakaoshughulikia migogoro ya kazi Zanzibar.
Walioapishwa ni Sisahau Rished Faki na Nemshi Abdallah.
Akizungumza baada ya kuwaapisha, Jaji Makungu alisema uteuzi huo utasaidia kushughulikia malalamiko ya wafanyakazi katika Mahakama ya Kazi.
Alisema malalamiko hayo yatashughulikiwa kwa ufanisi zaidi ili haki itendeke kati ya mlalamikaji na mlalamikiwa.
Aliwataka wasuluhishi hao kutenda haki katika majukumu yao ya kazi bila kuwa na upendeleo.
Kamishna wa kazi Zanzibar, Kubingwa Mashaka Simba, alisema jumla ya malalamiko 102 ya wafanyakazi yameripotiwa kwa mwaka 2013/3014 kati ya hayo, 59 yalipatiwa usuluhishi.
Alisema kuwa migogoro mingi wanayopokea kwa wafanyakazi ni tuhuma za wafanyakazi kufukuzwa kazi, wizi na kukatishwa mikataba kazini.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment