Aliyasema hayo wakati akifunguwa mkutano wa majaji, wanasheria na mahakimu kuhusiana na sheria na kanuni za uchaguzi katika kusimamia malalamiko ya walalamikaji.
Alisema baada ya uchaguzi mkuu kesi nyingi za wagombea ambao hawajaridhika na matokeo hufikishwa mahakamani, hivyo ni vyema kuzingatia miongozo ya Katiba ya Zanzibar ili kutoa maamuzi sahihi bila upendeleo.
“Hatua hiyo itaweza kuondoa dhana iliyojengeka kwa jamii kuwa mahakimu na majaji wanatumiwa na vyama vya siasa, jambo ambalo linaweza kuleta mivutano,” alisema Makungu.Aliwahimiza majaji na mahakimu hao kutorejea makosa yaliofanyika mwaka 1995, baada ya uchaguzi mkuu katika kusimamia malalamiko ya wagombea wa uchaguzi na kwamba mahakama ziligeuzwa kuwa majukwaa ya kisiasa na mahakimu na majaji wakaingia katika mlengo huo.
Aaidha, aliwataka kusimamia haki hasa katika wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu ili haki hiyo iweze kutendeka.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha, alisema jambo la kuzingatia kwa walengwa wa mkutano huo ni kufuata usimamizi imara wa kisheria ili wadau wa uchaguzi kuwa na imani na tume pamoja na mahakama.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment