SHULE mbalimbali za sekondari za bweni zinazomilikiwa na Serikali zimefungwa kutokana na kukosa chakula.
Uchunguzi uliofanywa na MTANZANIA umebaini takribani kwenye mikoa yote kuna shule zimefungwa na nyingine ziko hatarini kufungwa kwa kukosa chakula.

DODOMA
Mkoani Dodoma Shule ya Sekondari Mpwapwa iliyopo katika Wilaya ya Mpwapwa ilitakiwa kufunguliwa tangu Aprili 8, lakini imeshindikana kutokana na ukosefu wa chakula.
Akizungumza na MTANZANIA, mkuu wa shule hiyo, Nelson Mbilinyi, alisema walifunga shule kwa ajili ya likizo fupi, lakini hadi sasa hawajajua ni lini watafungua kutokana na tatizo hilo.
“Hadi sasa hatujajua tutafungua lini, lakini leo tuliambiwa kutakuwa na kikao na Ofisa Elimu wa Mkoa (REO) ndipo tutapata uhakika lini tutafungua shule,” alisema.
Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Msalato iliyopo katika Manispaa ya Dodoma, Mwasi Chibuni, alisema licha ya wanafunzi kuendelea na masomo, hali ya chakula si nzuri.
Alisema shule yao haijafungwa, lakini wanaendelea kuona chakula kitaishia wapi ndipo wachukue uamuzi.
“Sisi hatujafunga, tunaendelea hivyo hivyo tunajikongoja ila kama tukishindwa tutafunga,” alisema.Mkoani Dodoma Shule ya Sekondari Mpwapwa iliyopo katika Wilaya ya Mpwapwa ilitakiwa kufunguliwa tangu Aprili 8, lakini imeshindikana kutokana na ukosefu wa chakula.
Akizungumza na MTANZANIA, mkuu wa shule hiyo, Nelson Mbilinyi, alisema walifunga shule kwa ajili ya likizo fupi, lakini hadi sasa hawajajua ni lini watafungua kutokana na tatizo hilo.
“Hadi sasa hatujajua tutafungua lini, lakini leo tuliambiwa kutakuwa na kikao na Ofisa Elimu wa Mkoa (REO) ndipo tutapata uhakika lini tutafungua shule,” alisema.
Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Msalato iliyopo katika Manispaa ya Dodoma, Mwasi Chibuni, alisema licha ya wanafunzi kuendelea na masomo, hali ya chakula si nzuri.
Alisema shule yao haijafungwa, lakini wanaendelea kuona chakula kitaishia wapi ndipo wachukue uamuzi.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa, alipoulizwa kuhusu tatizo hilo la ukosefu wa chakula shuleni, alisema hana taarifa vizuri na kwamba atalisemea suala hilo leo atakapowasiliana na maofisa elimu kutoka wilaya zote.
TABORA
Mkoani Tabora, shule nne zimefungwa kutokana na wazabuni kusitisha huduma kutokana na kuidai Serikali zaidi ya Sh bilioni 1.5 za chakula walichokisambaza kwa shule mbalimbali.
Mapema mwezi Februari mwaka huu, ofisi ya
katibu tawala mkoa wa Tabora iliandika barua kwenda Tamisemi ikielezea ukubwa wa madeni ya wazabuni na yasipolipwa watasitisha huduma kama
ilivyotokea hadi shule zimefungwa.
Sekondari zilizofungwa ni Kazima ambayo wanafunzi wote wamerudishwa makwao isipokuwa wale wa kidato cha sita ambao wamepewa maelekezo ya kuwa wavumilivu kwani watabaki wakijiandaa kwa ajili ya kufanya mitihani.
Baadhi ya wanafunzi waliorudishwa makwao kutoka Shule ya Sekondari Kazima, wamesema walipewa taarifa kwa mdomo na walimu wao, kwamba
watatakiwa kurudi shuleni hapo Aprili 24 ama watakapotangaziwa vinginevyo.
Shule nyingine iliyofungwa ni Sekondari ya Wavulana Tabora ambapo kwa mujibu wa mwalimu ambaye hakutaka kutaja jina lake, wanafunzi wote wamerudishwa majumbani kwao na kubakishwa wa kidato cha sita tu wanaojiandaa kwa mitihani yao ya mwisho.
Kwa mujibu wa mwalimu huyo, shule hiyo kongwe mkoani Tabora na nchini kwa ujumla yenye zaidi ya wanafunzi 700, imebakisha 131 wa kidato cha sita pekee.
Sekondari nyingine ambazo pia zimefungwa kutokana na kadhia hiyo mkoani humo ni pamoja na Milambo na Tabora wasichana ambazo idadi ya wanafunzi waliorudishwa makwao haijafahamika.

MTWARA
Katika Mkoa wa Mtwara, taarifa zinasema shule za sekondari zilizopo wilayani Masasi tayari zimefungwa kutokana na hali hiyo.
Shule hizo zimetajwa kuwa ni Ndanda Boys, Masasi Girls, Chidya na Ndwika.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, MTANZANIA lilishuhudia baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wavulana Ndanda wakirudi majumbani kwao baada ya kufungwa.
Mmoja wa wanafunzi hao, Faudy Ngunguye anayesoma kidato cha tano, alisema wamerudishwa nyumbani baada ya shule kukosa chakula.
Lakini Ofisa Elimu Mkoa wa Mtwara, Karugendo Majidu, aliiambia MTANZANIA kuwa anatambua uwepo wa uhaba wa chakula katika shule hizo, lakini hana taarifa za kufungwa.
Majidu alisema alifanya kikao na wazabuni wanaohudumia shule hizo ambao mwanzoni walisema hawawezi kuendelea kutoa huduma, lakini baadaye walikubali kuendelea kutoa chakula.
“Kama kuna shule imefungwa labda ni kwa ajili ya likizo fupi ya sikukuu tu, lakini hadi sasa sina taarifa ya shule kufungwa, labda ongea na Ofisa Elimu Sekondari wa Wilaya ya Masasi anaweza kutoa taarifa sahihi zaidi,” alisema.
Alipoulizwa Ofisa Elimu Sekondari Wilaya ya Masasi, Paula Nkane, alisema shule hizo hazijafungwa bali zilikuwa kwenye likizo fupi ambayo inaisha leo.
Akizungumzia taarifa iliyotolewa na wanafunzi wa kidato cha tano katika sekondari ya Ndada, alisema walikuwa wamebaki shuleni wakati wa likizo, hivyo kutokana na kutokuwapo kwa chakula cha kutosha wamerudishwa nyumbani hadi shule zitakapofunguliwa.
“Hilo tatizo mimi silijui ila ninachojua wanafunzi wa kidato cha tano walitakiwa kuondoka shuleni wakati wa likizo kwakuwa chakula kisingeweza kuwatosha wao na kidato cha sita ambao wako karibuni kufanya mitihani,” alisema Nkane.

MWANZA
Katika Mkoa wa Mwanza, wazabuni wa vyakula mashuleni wametishia kugoma kutokana na Serikali kushindwa kulipa deni la Sh milioni 800.
Baadhi ya wazabuni hao wameieleza MTANZANIA kuwa wamekuwa wakidai fedha hizo kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo, huku Serikali ikiwapa ahadi hewa.
Mmoja wa wazabuni anayetoa huduma katika shule za sekondari za Bwiru wasichana na wavulana, ambaye hakutaka kutajwa jina lake gazetini, alidai kuwa anadai Sh milioni 300 katika shule hizo baada ya kutoa huduma ya chakula.
Shule ya Sekondari Mwanza, iliyopo katika Wilaya ya Nyamagana inadaiwa na mzabuni kiasi cha Sh milioni 116, ambazo ameshindwa kulipwa kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo.
“Ni kweli tunadaiwa kiasi hicho cha fedha na mzabuni huyo, Serikali imeshindwa kutuma fedha za kuwalipa wazabuni hao kwa wakati, endapo watasitisha huduma hawa wanafunzi itabidi tuwarejeshe makwao,” alisema mmoja wa walimu wa shule hiyo kwa sharti la kutotajwa jina lake.
Shule nyingine ambazo zinadaiwa na wazabuni ni Sekondari ya Nsumba pamoja na Ngaza, ambapo taarifa za uhakika zinaeleza kuwa kwa ujumla wake zinadaiwa zaidi ya Sh milioni 300.
Ofisa Elimu Sekondari katika Jiji la Mwanza, Emmanuel Katemi, alisema hawezi kulizungumzia suala hilo kwa kuwa linashughulikiwa na Serikali.

ARUSHA
Mkoani Arusha nako hali si shwari baada ya shule za Ilboru, Longido, Engutoto, Makuyuni na Kisimiri kudaiwa kuwa katika hali mbaya kutokana wazabuni kudai mamilioni ya fedha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Daud Ntibenda, alisema leo anatarajia kupata ripoti kamili juu ya hali ya chakula katika sekondari za Serikali mkoani humo.
“Nimesikia jana taarifa hizo, kwa sasa sina taarifa kamili, tayari nimemuagiza Ofisa Elimu wa Mkoa aniletee ripoti kamili ya suala hilo ofisini kwangu,” alisema Ntibenda.

MBEYA
Mkoani Mbeya, Shule ya Sekondari ya Iyunga, inatarajiwa kufungwa leo, kutokana na ukosefu wa chakula.
Shule hiyo ya wavulana yenye zaidi ya wanafunzi 900 wa kidato cha kwanza hadi cha sita, licha ya kufunguliwa hivi karibuni baada ya likizo ya Sikukuu ya Pasaka kwisha, kuna kila dalili ikafungwa kutokana na tatizo hilo.
Mkuu wa Shule hiyo, Mwalimu Edward Mwakimwa, alikiri kukabiliwa na uhaba wa chakula na kusema tayari uongozi wa shule kwa kushirikiana na Serikali ya Mkoa unaendelea na mchakato wa kuhakikisha chakula kinapatikana kwa wakati.
“Shule imeishiwa chakula kabisa kwani hata stoo zetu ni nyeupe, lakini tuna matumaini ya kupata chakula,” alisema.
Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Mariamu Mtunguja, alisema Serikali inalishughulikia tatizo hilo na kuhakikisha kwamba leo chakula kitakuwa kimepelekwa kwenye shule zote ambazo hazina chakula.

No comments :
Post a Comment