Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, April 1, 2015

Vitambulisho vyachafua hali ya hewa Barazani

  • Mzozo mkubwa uliibuka wakati wa kuchangia hoja hiyo wakati wajumbe wa CCM na CUF walipoanza kutupiana vijembe na maneno makali huku kila upande ukivutia kwake.
Zanzibar. Hali ya hewa katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar ilichafuka jana baada ya hoja binafsi kuhusu kuwapo kwa urasimu na ucheleweshaji wa kutolewa Vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi (Zan ID) iliyowasilishwa na Mwakilishi wa Ole (CUF), Hamad Masoud Hamad .
Mzozo mkubwa uliibuka wakati wa kuchangia hoja hiyo wakati wajumbe wa CCM na CUF walipoanza kutupiana vijembe na maneno makali huku kila upande ukivutia kwake.
Kilele cha mzozo huo kilikuwa pale Mwakilishi wa Kwamtipura(CCM), Hamza Hassan Juma alipoamua kuichana nakala ya hoja hiyo baada ya kumaliza kuchangia jambo lililosababisha mvutano mkubwa kiasi cha kumlazimu Spika wa Baraza, Pandu Ameir Kificho kuahirisha kikao.
Awali, akiwasilisha hoja yake, Hamad aliitaka Serikali itoe ufafanuzi wa kina kuhusu ucheleweshaji huo na kutaka kila Mzanzibari apewe kitambulisho bila usumbufu wowote.
Akichangia hoja hiyo, Hamza alisema inashangaza hoja hiyo ikiwasilishwa wakati huu nchi ikielekea katika Uchaguzi Mkuu Oktoba na kusema hoja hiyo imesukumwa na nguvu za kisiasa kuliko ukweli na uhalisia.
“Hoja hii Mheshimiwa Spika imekosa msingi na nguvu ya hoja, imejaa taswira ya kisiasa na propaganda, Baraza lisikubali vyombo vingine vivunje sheria, kama kukosa Zan ID ni mtaji wa kushinda na kushindwa, CCM haina jimbo hata moja kiswani Pemba,” alisema.
 Alipomaliza alisema haungi mkono hoja hiyo na kisha kuichana nakala yake aliyokuwa nayo akisema imekosa mantiki na ushahidi wa kimaudhui.
Mwakilishi huyo alikwenda mbali na kusema CCM haikutaka iwepo Serikali ya Umoja wa Kitaifa, bali ilishawishiwa kwa nia njema na Rais mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume.
Mwakilishi wa Ziwani (CUF), Saleh Nassor Juma alisema ni mshangao kuona Wamakonde wakipewa Zan Id huku Wazanzibari wenyewe wakinyimwa bila ya sababu za msingi na kuitaka Serikali idhibiti jambo hilo kabla halijaleta mvutano.
Hata hivyo, Mwakilishi wa Chumbuni (CCM), Machano Othman Said alisema kwenye jimbo lake kuna watu wengi wanaolazimisha kuandikishwa kwa hila wakati si wakazi na alipofuatilia alibaini si wakazi halali.
Mwakilishi wa Kojani, Hassan Hamad Omar alisikika akimtolea maneno makali Mwakilishi wa Chwaka, Issa Haji Gavu na kutaka kumvaa baada ya kumkuta akizungumza na Mwakilishi wa Kiwani, Hija Hassan Hija na Mwakilishi wa Ziwani, Nassor Saleh Juma lakini kabla tafrani hiyo haijakolea, polisi waliokuwapo waliwatuliza.
Akitoa maelezo kwa niaba ya Serikali, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud Mohamed alisema hakuna taarifa za kutosha iwapo Zan ID hazitolewi na kusema kwamba iwapo wapo watu wanaodai kunyimwa vitambulisho hivyo wanayo haki ya kupanda ngazi za juu ili kupata haki yao.
“Kila mwananchi ana haki ya kupata kitambulisho bila kupuuzwa, ikitokea mkurugenzi wa usajili wa vitambulisho au waziri anashindwa kutimiza jambo hilo, mtu ana haki ya kwenda mahakamani.”

No comments :

Post a Comment