Waziri wa Ardhi Maji Nishati na Makaazi, Mhe Ramadhani Abdalla Shaban akizungumza na Wanawanchi wanaoishi katika Nyumba za Maendeleo Unguja ambo wamepewa nyumba hizo na Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, Akitowa tamko kuwa kwa wale waliopewa nyumba hizo na Mzee Karume wataendelea kukakaa katika nyumba hizo bila ya kulipa Kodi na wale waliorithi kwa Wazazi wao watalipa Kodi ya nyumba hiyo. mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa jengo la sanaa rahaleo Zanzibar.
Wakaazi wa nyumba za maendeleo Zanzibar wanaoishi katika nyumba hizo walizopewa na Mzee Karume wakiwa katika mkutano huo na Waziri na Viongozi wa Idara ya Nyumba Zanzibar kupata muafaka waka wa suala lao.
Viongozi wa Wizara ya Ardhi wakimsikiliza Waziri Shabani akizugumza wakati wa mkutano huo. wakwanza Mkurugenzi wa Idara ya Nyumba Ndg Abdalla Mwinyigogo na Naibu Waziri wa Wizara hiyo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Ndg Mustafa Aboud Jumbe na Mama Fatma Karume wakifuatilia mjadala wakati wa mkutano huo na Wakaazi wa Nyumba za Maendeleo Zanzibar waliopewa na Marehemu Mzee Karume.
Wakaazi wa nyumba hizo wakifuatilia mjadala huo.
Mama Fatma Karume akizungumza wakati wa mkutano huo wa wananchi waliopewa nyumba kwa ajili ya makaazi na Marehe Mzee Karume kwa makaszi yao
Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali wakifuatilia mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa jengo la sanaa rahaleo Zanzibar.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardh Zanzibar Ndg Mustafa Aboud Jumbe akizungumza wakati wa mkutano huo na Wananchi waliopewa nyumba za Maendeleo na Mzee Karume kupata ufumbuzi wa matatizo yao waliokuwa wakidai kwa Wizara.
Waakaazi wakifuatilia Mkutano huo na Waziri Shabani.
Ustadh. akisoma dua baada ya kumalizika kwa nmkutano huo uliowakutanisha Wananchi wanaokaa nyumba za Maendeleo waliopewa na Mzee Karume kwa kuishi Zanzibar.
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema kuwa wananchi waliopewa nyumba za maendeleo za Serikali na Rais wa kwanza wa Serikali ya Zanzibar Sheikh Abeid Aman Karume wataendelea kuishi bure lakini watakapokufa wazee hao warithi wao watalazimika kulipa kodi kama Serikali ilivyoagiza.
Hayo yamesemwa leo katika ukumbi wa jengo la wasanii liliopo Rahaleo Mjini Zanzibar na Waziri wa Ardhi, Makazi, Maji na Nishati Mhe. Ramadhani Abdalla Shaabani wakati alipokuwa akizungumza na wakaazi wa nyumba hizo.
Amesema kuwa watoto wa wamiliki wa nyumba hizo wataendelea kuishi humo bila ya kubughudhiwa na mtu yoyote na jambo la muhimu ni kufuata agizo la Serikali juu ya kuzitunza na kufuata sheria zilizowekwa ili nyumba hizo ziweze kudumu kwa muda mrefu.
Amesema Serikali ya Mapinduzi tayari imeshapitisha maamuzi baada ya kukutana katika vikao vyake na kuamua kuwa wakazi hao pamoja na wazee wao watakaa ndani ya nyumba hizo bila kulipa kodi lakini kwa upande wa warithi watalazimika kulipa kodi iliopangwa na Serikali ambayo itaaza rasmi ifikapo mwezi wa saba mwaka huu.
“Uamuzi wa Serikali kwa watu waliothibitika kupewa nyumba na Mzee Abeid Amani Karume wataendelea kukaa bure, lakini mara tu watakapo kufa wazee hawa warithi wao watalazimika kulipa kodi na huo ndio uamuzi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar” aliesma Waziri huyo.
“Uamuzi wa Serikali kwa watu waliothibitika kupewa nyumba na Mzee Abeid Amani Karume wataendelea kukaa bure, lakini mara tu watakapo kufa wazee hawa warithi wao watalazimika kulipa kodi na huo ndio uamuzi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar” aliesma Waziri huyo.
Aidha amewataka wananchi wanaokaa katika nyumba hizo kwenda kuchukua fomu za mikataba kuanzia sasa na kusisitiza kuwa serikali itaendelea kuenzi juhudi za Mwanapinduzi huyo na kuzilinda, kuzienzi na kuthamini mchangowake kwa Taifa la Zanzibar.
Nae aliyekuwa Mke wa Rais wa kwanza wa Zanzibar Mama Fatma Karume amesema kuwa Mzee Karume katika uhai wake aliishi miaka saba tu baada ya Mapinduzi ambapo alijenga nyumba za maendeleo na aliwapa watu wasiojiweza kimaisha kukaa nyumba hizo, lakini leo hii kuna watu wanaojaribu kuwapotosha watoto wao kukaa humo bila ya malipo ya kodi ameongeza kwa kusema kuwa kwa hivi sasa karibu ulimwengu mzima wananchi wanakaa katika nyumba za serikali kwa kulipia kiwango kidogo cha kodi.
Nae mmoja wa wakaazi wa nyumba hizo za maendeleo Bi Zamzam amesikitikia kuwepo kwa kodi hiyo hivi sasa na kusema kuwa yeye itamwiya vigumu kulipa kwani hali yake ni mzee, masikini, na hana kazi ya kufanya, hivyo serikali iliangalie na hilo kwa watu wenye hali kama yake kwa kuwasaidia juu sualazima la ulipaji.
Chanzo: Zanzinews
No comments :
Post a Comment