Kauli hiyo aliitoa jana mjini hapa alipohutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Ndege mjini hapa.
Alisema ndiyo maana ACT- Wazalendo inaamini katika misingi ya Nyerere inayoleta usawa wa kidemokrasia na kuimarisha uchumi wa kila Mtanzania.
“Mwalimu Nyerere aliipenda Morogoro kwa kuigeuza kuwa mkoa wa viwanda lakini leo hii viwanda vya sukari asilimia 50 hapa na hakuna kiwanda kipya cha sukari tofauti na alivyovijenga Mwalimu.
Alisema pamoja na kujengwa viwanda hivyo bado vimekuwa vikiwanyonya wakulima wa miwa na hivyo kusababisha kilimo chao kutofaidisha wakulima wa miwa kama inavyofanyika kwenye bei na hawana haki ya kujua thamani ya miwa yao.
Kutokana na hali hiyo alisema chama cha ACT-Wazalendo kinataka kupiga marufuku uagizaji wa sukari bila kodi, huku akishauri kuanzishwa kwa viwanda vidogo vya miwa na wananchi wanaolima miwa wote kuwa na hifadhi ya jamii kuweza kuboresha maisha yao ya sasa na baadaye.
Zitto ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), alisema Mkoa wa Morogoro unazalisha nusu ya sukari nchini.
“Hata hivyo sukari nchini haitoshi kwani uwezo wetu ni kuzalisha tani 300,000 wakati mahitaji ni tani 500,000. Ili kuhakikisha bei ya sukari inakuwa himilivu ACT inapendekeza viwanda vya sukari kupewa bei nafuu ya umeme kama ruzuku,” alisema.
Akizungumzia jinsi Mkoa wa Morogoro unavyochangia katika Pato la Taifa (GDP), Zitto alisema unashika nafasi ya sita kati ya mikoa 21 ya Tanzania Bara lakini bado upo chini kwa maendeleo. 2014, ambao walitumia hesabu za uchumi za 2012
“…lakini Mkoa wa Morogoro upo chini kwenye maendeleo ya watu wake ambapo unashika nafasi ya 11. elimu ni changamoto kubwa ambapo katika kila watu 100 wa wa mkoa huu ni watu wanane tu ndiyo wana elimu ya sekondari,” alisema.
No comments :
Post a Comment