Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum Haji Omar Kheir (kushoto) akiwa na Washauri wa Rais Balozi Mohammed Ramia Abdiwawa,Abrahman Mwinyi Jumbe na Burhani Saadat Haji wakiwa ni miongoni mwa Viongozi waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Mkuu wa Wilaya mpya ya Magharibi "B" Ayoub Mohammed Mahmoud Ikulu Mjini Unguja leo.[Picha na Ikulu.]
Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad (kulia) Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu (katikati) na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis wakiwa hafla ya kuapishwa Mkuu wa Wilaya mpya ya Magharibi "B" Ayoub Mohammed Mahmoud Ikulu Mjini Unguja leo kazi iliyofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.[Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Ayoub Mohammed Mahmoud kuwa Mkuu wa Wilaya Mpya ya Magharibi "B" katika Mkoa wa Mjini Magharibi hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo na kuhudhuriwa na Viongozi mbali mbali,(Picha na Ikulu.)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi hati ya kiapo Ayoub Mohammed Mahmoud baada ya kumuapisha kuwa Mkuu wa Wilaya Mpya ya Magharibi "B" katika Mkoa wa Mjini Magharibi hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo na kuhudhuriwa na Viongozi mbali mbali,(Picha na Ikulu.)
STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 13 Mei, 2015
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein leo amemuapisha Ndg. Ayoub Mohammed Mahmoud kuwa Mkuu wa Wilaya Mpya ya Magharibi ‘B’ katika mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.
Kabla ya kuteuliwa kuwa mkuu wa wilaya hiyo mpya, ndg. Ayoub alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Magharibi ambayo sasa kwa mujibu wa mabadiliko ya kiutawala yaliyofanyika hivi karibuni imegawanywa katika wilaya mbili za Magharibi ‘A’ na Magharibi ‘B’.
Hafla hiyo fupi iliyofanyika Ikulu ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad.
Wengine ni pamoja na Jaji Mkuu Mheshimiwa Othaman Makungu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Mheshimiwa Haji Omar Kheri, Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Maalim Abdalla Mwinyi Khamis.
No comments :
Post a Comment