Kafulila alisema hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam, wakati wa kikao cha Kamati ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara, iliyokutana na Wizara ya Fedhana mamlaka zake.
Alisema, kwa mujibu wa maelezo ya Gavana wa Benki Kuu (BoT), Profesa Benno Ndulu, sababu za kushuka kwa shilingi ni kuimarika kwa dola ya Marekani na kusababisha sarafu zote duniani kuathirika katika mbadilishano na dola.
Aidha, sababu nyingine ni uhaba wa dola uliosababishwa na kukosekana kwa fedha za wafadhili.
Kafulila alisema misaada iliyokuwa inatarajiwa kutoka kwa wahisani imekwama kutokana na sakata la Escrow.
Alisema mikopo ya kibiashara ambayo Tanzania ilikuwa ikitarajia kupata dola milioni 800, imekatwa na kutolewa dola milioni 300, tafsiri inayoonyesha kuwa Tanzania haiaminiki.
Alisema fedha za wafadhili zaidi ya Sh. tirioni 1.0, sawa na dola milioni 740, hazijaidhinishwa kupewa Tanzania na mwaka jana Wizara ya Fedha ilisema zitaidhinishwa Desemba, mwaka jana.
“Mwaka huu wanazungumzia labda zitasainiwa Septemba tafsiri yake ni kwamba hiyo hela ambayo ni sawa na tirioni 1.5 haitaletwa hadi hatua zichukuliwe kwenye jambo la Escrow,” alisema.
Hata hivyo, alisema mikopo ya biashara ya dola milioni 500-800 iliyoahidiwa kuletwa imekwama kwa sababu ya sakata la Escrow.
Alisema tatizo la serikali ni kusema hatua zimechukuliwa wakati, IPTL inalipwa zaidi ya Sh bilioni 5 kila mwezi, kama tozo ya uzalishaji (Capacity Charge).
“Fedha ambayo ina mgogoro inaendelewa kulipwa, hapo ni hatua gani iliyochukuliwa,” alihoji na kuongeza ndiyo maana nilikuwa ninabisha kuwa hili sakata la IPTL halijafungwa kwa sababu hakuna hatua zilizochukuliwa.”
Aliongeza kuwa zaidi ya Sh. bilioni 60 analipwa Habirnder Seth Singh kila mwaka wakati ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), inaeleza aligushi nyaraka, wakati kosa la kugushi ni la jinai.
Kwa upande Gavana wa Benki Kuu, Ndulu alisema thamani ya Shilingi ya Tanzania dhidi ya dola ya Marekani ilishuka katika soko la jumla la fedha za kigeni kutoka Sh 1,318 kwa dola moja mwezi Januari 2010 na kufikia kiwango cha Sh 1,543 kwa dola moja, mwezi Juni 2011.
Aidha, alisema katika kipindi hicho, thamani ya shilingi katika soko la rejareja ilishuka kutoka shilingi 1,333 kwa dola moja ya Marekani na kufikia shilingi 1,547. Kushuka kwa thamani ya shilingi kulichangiwa na mfumuko mkubwa wa bei pamoja na mauzo hafifu nje ya nchi hasa kufuatia mdororo wa uchumi duniani.
Aliongeza kuwa thamani ya shilingi ilishuka kwa kasi zaidi kati ya mwezi Juni 2011 hadi Oktoba 2011 kufuatia baadhi ya washirika wa soko la fedha za kigeni kucheza kamari/kufanya biashara ya dola kwa lengo ya kujinufaisha.
Kufuatia hali hiyo, hatua mbalimbali zilichukuliwa na Benki Kuu ikiwa ni pamoja na kuongeza viwango vya akiba ambavyo mabenki yanatakiwa kuhifadhi Benki Kuu (SMR) kutoka asilimia 20 mpaka asilimia 40 kwa amana za serikali.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
No comments :
Post a Comment