Written by abdisalum
Kuna habari tumepata kuwa jengo la zamani la PBZ (benki ya watu wa Zanzibar) pale Shangani limeuzwa au tunavyosikia limekodishwa kwa wawekezaji wa Uturuki. Uza Uza inaendelea mpaka tumaliza kila kitu. Jengo hili zamani sana lilikuwa la Wahindi na maarufu wake ilikuwa bank na ndio hiyo ‘jetalela’ kama sikosei.
Jengo hili lenye thamani kubwa sana limeshauzwa chini ya utawala wetu wa Dr.Ali Mohammed Shein. Mbao zake ni msaji mtupu, na ndio hasa inayotakiwa.
Wale wanaofanya kazi mle, ofisi ya Mrajisi wa Vizazi+Vifo na taasisi nyengine wametakiwa waondoke mara moja. Na hivi sasa, wanahamia ofisi yao mpya ya Wizara ya Katiba na Sheria iliyopo Mazizini. Tukumbuke kuwa hawa wamehamishwa pale Mambomsiige takriban miaka michache tu iliyopita, sasa wanapigwa tena uhamisho. Process hii na hama na kuhamia, imeigharimu serikali pesa nyingi sana, lakini muhimu imepoteza nyaraka muhimu na kumbukumbu muhimu za nchi.
* Kidumu Chama cha Mapinduzi.Sina hakika kama uuzaji huu umezingatia taratibu za kiserikali za mauzo/au any procurement procedures na pesa hizi zimeingia wapi, au ndio ile aliyosema Dr.Shein kuwa “serikali haihojiwi wala kuulizwa inapouza chake”. Hiyo ndio ‘check and balance’ ya Dr. Shein. Hiyo ndio ‘good governance’ ya Dr.Shein.
Ardhi imeuzwa, majengo yote yanauzwa na mpaka misikiti itauzwa hapa Zanzibar ili kujenga hoteli za kitalii na kupata pesa za kigeni??
Nasikia hata ile iliyokuwa wizara ya katiba/sheria pale karibu na skuli ya Tumekuja nayo imeuzwa.
Tukumbuke kuwa zote hizi zipo chini ya Mheshimiwa Ababakar Khamis Bakari (CUF) haki sawa kwa wote. Hivi kwlei ndio hajui au haoni au naye xxxx chake.
Note: Rasmi ni kuwa pia hoteli ya Bwawani imeuzwa au imeingzwa ubia na serikali – hiyo angalau sio siri imetamkwa rasmi na Rais mwenyewe Dr.Ali Mohammed Shein alipolifunga rasmi BLW mwaka huu. Kidumu Chama cha Mapinduzi. UKAWA Oyeeee! Hakiiiiiii……….?
Nchi inakwenda arijojo, na sisi tumekaa tunashangilia siasa tu za kupiga kofi na kucheza ‘mguu mbele, mguu nyuma’ au daima, daima , daima na kidumu……… Maalim Seif upo wapi? na ile pale Park Hyatt, vipi mbona kimya —- naona nyotee mmeufyata.
Siku nyingi nimehajir katika ukumbi, ila ninaona na kusoma — msione kimya/nilikuwa ninalimia mikarafuu yangu kule Chonga na Mzambarau takao, karibu na Bahanasa.
No comments :
Post a Comment