zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, July 22, 2015

Kilichowafika Bilal, Pinda, Jaji Ramadhani, Sitta

SABABU za kukatwa kwa viongozi waandamizi na watu mashuhuri kwenye mchakato wa kuwania urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) zimefahamika. Kwenye mchakato huo ambao wanachama 42 walijitokeza, viongozi wa juu kama Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Ghalib Bilal, hawakuweza kuingia hata kwenye tano bora. Raia Mwema limeelezwa sababu kuu tatu ambazo zilitumika kuwaengua baadhi ya viongozi mashuhuri na wakuu kwenye serikali. Umri Vyanzo vya kuaminika kutoka ndani ya Kamati ya Usalama na Maadili na kisha Kuu ya CCM (CC) vimeliambia gazeti hili kuwa chama hicho kiliamua kuwa mgombea wake anatakiwa kuwa na umri mdogo kuliko Rais Jakaya Kikwete. Hiyo ni kwa sababu, Kamati Kuu iliona kuwa taifa lina idadi kubwa ya vijana na hivyo ni vema uchaguzi wao ukazingatia suala la umri ili kuvutia kura za kundi hilo. Gazeti hili limeambiwa kuwa ndiyo sababu wagombea wote waliokuwa na umri zaidi ya miaka 65 walikatwa mapema. Viongozi waliokatwa majina yao kutokana na suala hilo na umri wao kwenye mabano ni Samuel Sitta (73), Jaji Augustino Ramadhani (70), Mizengo Pinda (67), Dk. Mohamed Ghalib Bilal (70), Dk. Augustine Mahiga (70) na Profesa Mark Mwandosya (66). Raia Mwema limeambiwa kuwa wagombea hao wote, japo walikuwa na sifa za uongozi, umri ungekuwa kikwazo kwao kwenye kukitafutia chama ushindi. “Mwenyekiti aliwaeleza wajumbe wa CC kuhusu mapendekezo hayo na yakakubaliwa. Si kawaida kwa viongozi wa juu kukatwa mapema lakini mara hii ilibidi iwe hivyo,” alisema mmoja wa wajumbe wa CC aliyezungumza na gazeti hili kwa masharti ya kutotajwa jina. Mgombea aliyepitishwa na chama hicho, John Magufuli, ana umri wa miaka 55, ambao ndiyo Kikwete alikuwa nao wakati alipopitishwa na chama hicho kuwania urais mwaka 2005. Makundi Kuna wagombea wengine, mfano ukitolewa wa Dk. Harrison Mwakyembe, Makongoro Nyerere na Sitta pia, ambao chama kiliamua kuwakata kwa maelezo kuwa wana makundi. Gazeti hili limeambiwa kuwa chama kilikuwa kimedhamiria kuwa mwaka huu kitasimamisha mgombea ambaye hana makundi. Mwakyembe na Sitta wamekuwa wakifahamika kama wabunge wapambanaji dhidi ya ufisadi na walikuwa mahasimu wa kisiasa na kundi lililokuwa likimwunga mkono Edward Lowassa. Magufuli, ambaye hatimaye amepitishwa na CCM kuwa mgombea wake, anafahamika kwa kutohusishwa na kundi lolote ndani ya chama hicho. Idadi ya wagombea Nje ya sababu hizo mbili rasmi zilizotolewa na CCM kuhusu kuwakata wagombea hao, wapo wanaoamini kuwa suala la idadi kubwa iliyojitokeza kuwania urais ilikuwa na maana yake. “CCM haiwezi kusema lakini haikuwa bahati mbaya kuwa watu 42 walijitokeza kutaka kupitishwa na chama kuwa wawania urais. “Kati ya waliojitokeza, kuna wengine wala hawakuwa na nia ila walishawishiwa na mfumo kuingia. “Lengo hapa lilikuwa kuwa utakapofika wakati wa kukatana majina, wakatwe pia viongozi wakubwa. “Viongozi wakubwa watakapokatwa, itakuwa vigumu kwa watu wengine kulalamika. Sasa kama Waziri Mkuu au Makamu wa Rais nao wamekatwa, nani atakayelaumu?” Kilisema chanzo hicho.
- See more at: http://raiamwema.co.tz/kilichowafika-bilal-pinda-jaji-ramadhani-sitta#sthash.vCP2qGET.dpuf

No comments :

Post a Comment