zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, July 23, 2015

KINGUNGE AFUKUZWE CCM!

Image result for kingunge ngombale mwiru
Muandishi Abdi Salum wa Mzalendo.net asema Kingunge nae afukuzwe kama CCM ilivyomfukuza Moyo!

Image result for hassan nassor moyo
Mzee Moyo aliefukuzwa CCM kwa kusema kweli!
    
TUJIKUMBUSHE NA HABARI ZA KUFUKUZWA KWA MZEE MOYO KUTOKA CCM!

Na Abdisalum
Mzee mwenzanu Hassan Nassor Moyo amefukuzwa CCM [yeye ni mwanachama NO.7] kwa kusema ukweli wa mambo na kuetetea kile kinachoonekana kuwa ni haki au matakwa ya wengi. Amefukuzwa na kikao dhalil kabisa, kikako cha wilaya kichama.Inashangaza sana. hapa nilitegemea kumuona Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, kada wa CCM mkongwe na kominist mkubwa aliyebaki TZ anaweza kunyanyua sauti na kusema hivi sivyo jamani. Tuache hayo!

Sasa, yamemkuta yeye mwenyewe. Ameona dhulma na kama alivyosema yeye mwenyewe kuwa vikao vya CCM vya kumtafuta na kumpata mgombea wa CCM ni ‘batil’. Neno zito hilo. Ina maana hata rais tutayempata atakuwa batil. Ndio maana yake.
Sasa, JE CCM ITAMFUKUZA KINGUNGE? PENGINE CCM KIWILAYA YA ILALA AU KIONONDONI IMFUKUZE BASI KWA KUKOSOA CHAMA, AU KUKOSA MAADILI? AU AMEONEWA MZEE MOYO KWA KUSEMA UKWELI, au kwa sababu ni Mzanzibari??

Sasa bado niko na wewe Mzee Kingunge. Kwa nini basi umekaa kimya wakati wa zoezi la uandikishaji w awapiga kura bara na zanzibar unaendeshwa kibatil batil? ndio hujui au halijakuhusu. Lowassa amekuumiza ila haya yetu huku hayakuhusu.

Hivi kweli Mzee Kingunge hujui kama hapa Zanzibar kuna bvijana less than 18 wameingizwa katika vikosi vya kupiga watu, janjaweed, au siku hizi wanavaa ninja (zombie). Hivi hujui kama daftari la wapiga kura Zanzibar limeharibiwa sana sana na ni batil, na huko bara kadhalika? Haya tunaomba uyaseme na tuyasikia. Tunakuamin, na tunataka uwe mtetezi wa haki, na tuibatilishe batil.

Usisahau Mzee mwenzangu kuwa wewe ndiye uliyekuwa mstari wa mbele kuikataaa GNU, serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar, mpaka siku ukiyozozana na Jussa na Jussa alikupa vidonge vyako pale Kibanda Maiti. Wewe ndiye ulieyesema GNU inamrejesha Jamshid na Hizbu itarudi.

Mzee Kingunge, mbona hueleweki? Hvi kwlei hujui kuwa waliomtema Lowassa si CCM ila ni jumuiya za kimataifa? kashfa zote yumo, pesa zote hizo ni za wafadhili, na TZ sasa haina tena misaada yoyote ile ila madeni kutoka China na Afrika Kusini, na wananchi ndio wanaoumia au hujui haya? Kwa kigezo cha CCM, Lowasa ndiye hasa anafaa, lakini mbele ya macho ya dunia — huyu siye na hafai kabisa kabisa. Mimi binafsi yangu, ninashangaa wewe Kingunge kumtetea mtu kama huyu, na Watanzania kumshabikia, ninaona ajabu kuwa kumuona Lowassa anachukua fomu ya kutaka kugombe Urais wa nchi. 


Na wewe Mzee unamshabikia tu….are you ok….? au vipi. Si Mwinyi, si Mkapa, si wewe Kingunge nyote kufanya kitu haki hamjui wala hamuwezi. Kama unao ubavu wa kusema na kutetea haki, naomba uzungumzie kuhusu janjawee na zombie wa Zanzibar, ambao nina hakika unajua kuwa wamepanga ushenzi na ujahil wa hali ya juu hapa. Waambie wenzako kuwa Hissene Habre anashtakiwa tayari, waambie wenzako kuwa TZ tayari inatiwa adabu kw akuwa ni kinara wa kula rushwa….haina tena misaada. Na yakitokea mauwaji Zanzibar mjue kuw adunia inatutazama na tayari inaangalia kwa jicho makini.

Nakutakia kazi njema Mzee mwenzangu Kingunge.


http://mzalendo.net/habari/kingunge-afukuzwe-ccm.html

No comments :

Post a Comment