zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, July 23, 2015

Mkutano wa NEC, vyama vya siasa wavunjika Dar.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Philip Mangula.
Mkutano  wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na vyama vya siasa kwa ajili ya kusaini maadili ya uchaguzi ya mwaka 2015 jana ulivunjika huku viongozi wa vyama wakiitupia lawama tume kwa kukosa umakini.
 
Mkutano huo ulianza jijini Dar es Salaam jana, lakini muda mfupi baadaye  ulishindwa kuendelea baada ya Mkurugenzi wa Nec, Julius Malaba, kumkaribisha Makamu Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar, Hamid Mahamoud Hamid, kusoma maadili ya uchaguzi ya mwaka huu.
 
Habari kutoka ndani ya kikao hicho zinaeleza kuwa kabla Jaji Hamid kusoma makabrasha yaliyokuwa yameandikwa maadili, Katibu wa Chama Cha Kijamii (CCK), Renatus Muabhi, alisimama na kuomba taarifa.
 
Muabhi baada ya kuruhusiwa alieleza kuwa vyama vya siasa havina imani na Nec kwa sababu imekiuka makubaliano ya awali ya kutakiwa kupeleka nakala zenye taarifa za maadili ya uchaguzi kwa vyama vya siasa ili viongozi wa vyama wasome na kuchambua kabla ya kufanyika mkutano huo.
 
“Tulikubaliana katika vikao vilivyopita kwamba  maadili haya tuletewe kwanza tuyasome, lakini leo hii mmetuita hapa na kutupatia kabla hatujasoma ili tusaini kinyume cha makubaliano yetu,” alisema.Muabhi alisema kutokana na Nec kukiuka makubaliano hayo, wanahisi kuna ajenda ya siri, hivyo hawatakuwa tayari kusaini hadi wapate fursa ya kusoma yaliyomo.
 
Naye Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Philip Mangula (pichani), alisema hayo ndiyo yalikuwa makubaliano ya vyama na tume na kubainisha mapungufu mengine kuwa ni ukosefu wa kurasa 13 ndani ya kabrasha lenye maadili lililowasilishwa kwa wajumbe.
 
“Tume mmetudhalilisha, inaonyesha hamjajipanga, mmetuita kusaini maadili wakati hakuna kurasa 13 humu, hii lazima watu wawajibike,” alisema Mangula.
 
Chanzo cha habari kutoka ndani ya mkutano huo kilieleza kuwa kutokana na hali hiyo, Mangula alishauri mkutano huo uahirishwe ili kutoa fursa kwa Nec kujipanga vizuri.
 
Kufuatia hali hiyo, Jaji Hamid aliwaomba radhi wajumbe kuahidi yatafanyiwa kazi mapungufu yaliyojitokeza.
 
Malaba akizungumza na NIPASHE alisema mkutano mwingine utafanyika Jumatatu ijayo. Julai 20, mwaka huu, tume hiyo iliwaandikia barua yenye kumbukumbu namba EA.75/162/08/56 makatibu wakuu wa vyama vya siasa kwa ajili ya kusaini maadili ya uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.

CHANZO: NIPASHE


No comments :

Post a Comment