Akizungumza na NIPASHE ofisi kwake, Ofisa Mtendaji Mkuu wa TGFA, Kapteni Keenan Mhaiki, alisema chama hicho kilifuata taratibu zote zinazohusiana na kukodi ndege hiyo na kusisitiza kwamba mtu au chama chochote kitakachohitaji huduma ya usafiri kinapata ndege hizo, lakini inategemea ratiba za viongozi wa serikali ambao huzitumia kwa safari mbalimbali.
“Hakuna mtu aliyenyimwa ndege ukiona hajapatiwa kunatokana na ratiba kuwa ngumu mara nyingine hutoa huduma ya usafiri timu za mpira zinaposafiri,” alisema Kapteni Mhaiki.
Aidha, alisema ndege hiyo hukodishwa bila upendeleo huku akisisitiza kwamba hakuna mtu au chama kilichowahi kukodi kikanyimwa.
Alisema TGFA itaendelea kufanya jitihada za kutoa elimu ya matumizi ya ndege za serikali kwa jamii ili kuondoa dhana potofu iliyojengeka kuhusu suala hilo.
Julai 19, mwaka huu Dk. Magufuli alitumia Ndege ya serikali aina ya Fokker F28 kwenda Mwanza kujitambulisha kwa wanachama.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment