zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, July 26, 2015

Tufundishe na tujifunze lugha za kigeni

Image result for learn foreign language
HAKUNA ubishi kwamba kuna tofauti kati ya mwanadamu aliyeishi maisha yake yote akifahamu lugha moja tu na mwengine ambaye amezungumza na kujifunza kutoka katika lugha zaidi ya moja.
Mtu kufahamu lugha zaidi ya moja kuna faida nyingi. Ukifahamu lugha nyingine, ina maana utakuwa na fursa ya kusoma na kusikia wengine wakizungumza kuhusu maarifa waliyonayo. Ukifahamu Kiingereza, ni rahisi kuwafahamu Waingereza na hivyo hivyo kwa mtu anayejua lugha nyingine miongoni mwa zile za kimataifa zinazofahamika.
Katika nyakati hizi tunahitaji kupata maarifa na ujuzi kutoka mataifa mbalimbali yaliyoendelea na yanayoendelea ili yatusaidie kuleta maendeleo yetu. Maarifa na ujuzi yanaweza kuwa katika maeneo ya elimu, afya, kilimo, viwanda, biashara, uchumi, n.k.
Maarifa hayo na ujuzi huo kutoka mataifa mengine kwa kawaida hupatikana kwa lugha za mataifa hayo; na kwa hiyo, ili tuyapate maarifa hayo na ujuzi huo, ni muhimu kuzijua lugha za mataifa hayo. Siyo rahisi kujifunza lugha za mataifa yote; lakini tunaweza kufundisha/kujifunza lugha mbili, tatu au nne za kigeni katika mfumo wetu wa elimu.
Mfano wa lugha tunazohitaji kufundisha/kujifunza ni pamoja na Kiingereza, Kifaransa, Kiarabu, Kihispania, Kichina na zinginezo.Lugha zetu za asili na lugha ya Kiswahili tusiziache, bali tuzijue sawasawa ili ziwe ni mwamba ambao juu yake tutajenga uwezo wa kujifunza lugha za kigeni. Kwanza kabisa, nadharia ya kujifunza lugha ya pili au ya kigeni inasema kwamba njia ya kujifunza lugha ngeni inapitia katika lugha zetu za kwanza au lugha za awali.

Pili, uzoefu wa kufundisha lugha za kigeni katika nchi zilizoendelea na zinazoendelea pia unakubaliana na nadharia hiyo. Tatu, lugha zetu za asili pamoja na Kiswahili ni utambulisho wa utaifa wetu. Utaifa wetu huu ndiyo unaotuwezesha tuwe sehemu ya mataifa.
Kwa maneno mengine, ni lazima tuwe taifa kwanza, ndipo tutajulikana kuwa sehemu ya mataifa mengine. Hatuwezi kamwe kuwa sehemu ya mataifa bila kuwa taifa kwanza! Kwa sababu hiyo, lugha zetu za asili na Kiswahili tusizipoteze.
Nahitaji kuweka msisitizo: sijasema tutumie mojawapo ya lugha hizi za kigeni kufundishia elimu yetu, la hasha. Nimesema tufundishe na tujifunze lugha hizi kama lugha za kigeni ili tuweze kushiriki maarifa na ujuzi unaopatikana katika lugha hizi na kutoka mataifa yenye lugha hizo.
Naweka msisitizo huo kwa sababu athari za kutumia lugha za kigeni kufundishia elimu tumeziona kwa miongo zaidi ya mitano hapa Tanzania. Athari hizo ni pamoja na elimu duni na tengefu (isiyo shirikishi) na inayotoa wasomi waliokariri bila kujifunza maarifa au kupata ujuzi na kudadavua au kusimamia ukweli.
Wasomi wanaozichukia au kutojifunza vizuri lugha zetu za asili pamoja na Kiswahili; na wasomi waliojifunza kwa Kiingereza kibovu na kujivunia hichohicho kwa kuamini kwamba, bora kibovu kuliko kukikosa kabisa wanafanya makosa makubwa sana.
Tunaweza kujifunza lugha kadhaa kwa kuzipanga kwa utaratibu maalumu katika mfumo wetu wa elimu. Kwa mfano: watoto wanapoanza shule za awali hadi miaka miwili ya shule za msingi wanaweza kuruhusiwa kutumia lugha za asili za eneo lao au lugha ya Kiswahili.
Hii ni miaka ya mpito kuelekea kutumia Kiswahili kujifunzia. Kuanzia darasa la tatu na kuendelea Kiswahili kinaweza kupangwa kutumika kufundishia masomo yote hadi vyuo vikuu. Kuanzia darasa la tano, Kiingereza kikaanza kufundishwa kama lugha ya kwanza ya kigeni, hadi kidato cha nne. Kifaransa kikaanza kufundishwa kama lugha ya pili ya kigeni kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne. Kidato cha tatu, Kiarabu, Kichina au Kispanyola kikaanza kufundishwa kama lugha ya tatu ya kigeni hadi kidato cha nne.
Kwa utaratibu huo, elimu yetu itakuwa imetoa fursa kwa wasomi kuhitimu wakiwa na maarifa na ujuzi zaidi kuliko sasa; wenye kufahamu Kiswahili na lugha za jamii zao kuliko sasa; wenye kufahamu Kiingereza vizuri zaidi kuliko sasa; na wenye uwelewa wa msingi wa lugha za kigeni zaidi ya moja kwa ngazi mbali mbali, jambo ambalo ni muhimu katika dunia ya leo.
Zaidi ya yote, wahitimu wa aina hii wataweza kushiriki kuanzia ngazi za jamii zao, ngazi za taifa, hadi ngazi za kimataifa. Mwenyezi Mungu na atuongoze kuimarisha yaliyo bora katika jamii zetu!

- See more at:http://raiamwema.co.tz/tufundishe-na-tujifunze-lugha-za-kigeni#sthash.CwQc5Ena.dpuf 

No comments :

Post a Comment