Mgombea urais kupitia CCM Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damiani Lubuva, wakati alipowasili ofisi hizo.
Mgombea urais kupitia CCM Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wanahabari baada ya kurudisha fomu.
MGOMBEA urais kwa tiketi ya vyama viwili, John Pombe Magufuli, leo amerudisha fomu ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
NEC iliwataka wagombea wote wa urais kupitia vyama vyote vya siasa kurudisha fomu leo Agosti 21 baada ya kuzunguka mikoa ya Tanzania kutafuta wadhamini, ambapo vyama vyote hivyo viwili vimeonekana kukidhi vigezo na kurudisha fomu hizo.
(PICHA: DENIS MTIMA/GPL)
Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi ndugu John Pombe Magufuri amerudisha fomu ya kugombea urais wa jamhuri katika ofisi za tume ya taifa ya uchaguzi (NEC) muda huu.
Katika tukio ambalo limekuwa na kivutio kikubwa kwa watumishi wa NEC, waandishi wa habari na wananchi waliokuwa wakipata huduma katika jengo la NEC ni kitendo cha mgombea huyo kuacha kutumia lift na kupanda ghorofa saba za jengo hilo kwa miguu.
Katika kile kilichoonekana kuwa ni kudhihirisha hali nzuri ya Afya yake, Magufuli amewataka viongozi wa CCM alioongozana nao katika tukio hilo nao washukr kwa ngazi kama yeye.
Magufuli pia alikubali ombi la waandishi la kupiga picha nae ya pamoja ya Ukumbusho kabla hajatangazwa rasmi kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
No comments :
Post a Comment