Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, August 7, 2015

Simbachawene: Sijawahi kuona mchakato wa uchaguzi CCM kama wa mwaka huu.

  Kampeni zimejaa kukashifiana, kudhalilishana, watu wanatukana wagombea wenzao mpaka chama chenyewe.

Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene.
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene, amesema hajawahi kushuhudia mchakato wa uchaguzi wa wawakilishi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu wa wabunge na madiwani wenye siasa za udhalilishaji kama uliyofanyika mwaka huu.
 
Simbachawene aliyekuwa mmoja wa wagombea wa ubunge Jimbo la Kibakwe mkoani Dodoma, alisema: "Binafsi nashukuru Mungu kwa kumpa ustahimilivu kiasi cha kutomshushia kipigo
mgombea mwenzangu yeyote wakati wa mchakato huo."
 
“Kampeni zimejaa kukashifiana, kudhalilishana, watu wanatukana
wagombea wenzao mpaka chama chenyewe. Yaani namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kutompiga mtu mpaka uchaguzi huu unakwisha,” alisema Simbachawene.
 
Alisema amekuwa Mbunge wa Jimbo la Kibakwe tangu mwaka 2000, akishiriki na kushinda chaguzi za ndani, lakini hakuwahi kushuhudia uchaguzi wenye siasa chafu kama ilivyokuwa katika uchaguzi wa mwaka huu."Baadhi ya wagombea walifanya kampeni kama vile ni wanachama wa vyama vya upinzani," alisema Simbachawene.
 
Simbachawene ambaye hata hivyo aliyetangazwa kuwa mshindi wa kinyang'anyiro hicho alijizolea kura 18,158.
 
Matokeo hayo yalitangazwa na Katibu wa CCM wa Mkoa wa Dodoma, Albert Mgumba.
 
Jumla ya makada wanane wa CCM waliwania nafasi hiyo katika jimbo hilo huku aliyemfuatia Simbachawene akiwa ni Gabriel Mwikola, aliyepata kura 6,901.
 
Simbachawene alisema inaelekea mfumo wa wanaogombea uongozi kwa kudhaminiwa na vyama vya siasa, sasa umepitwa na wakati.
 
Alisema Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977, inaelekeza mtu anayetaka uongozi kwa kupigiwa kura na wananchi, awe mwanachama wa chama cha siasa, sharti ambalo hata hivyo, alisema limeanza kupoteza umuhimu wake ndani ya jamii ya Kitanzania.
 
Alisema ni bora Katiba inayopendekezwa ambayo ina kipengele kinachoruhusu mgombea binafsi ipitishwe ili wananchi wapate fursa ya kupima ubora wa aina mbili za viongozi; wanaotokana na vyama vya siasa na wale wanaojidhamini wenyewe.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment