Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, August 30, 2015

Uzinduzi wa Kampeni ya Chadema Jangwani

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa pamoja na Mgombea mwenza, Mh. Juma Duni Haji wakiwasili kwenye viwanja vya Jangwani Jijini Dar es salaam, kulikofanyika Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho, leo Agosti 29, 2015. PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.
 Umati wa wakazi wa Jijini Dar es salaam, ukiwa umefurika kwa wingi kwenye viwanja vya Jangwani kuwalaki Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa pamoja na Mgombea mwenza, Mh. Juma Duni Haji, walipokuwa wakiwasili viwanjani hapo, kulikofanyika Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho, leo Agosti 29, 2015.
Wafuasi wa Vyama vinavyounda UKAWA wakiwashangilia Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa pamoja na Mgombea mwenza, Mh. Juma Duni Haji, walipokuwa wakiwasili viwanjani hapo, kulikofanyika Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho, leo Agosti 29, 2015.
Wafuasi wa Vyama vinavyounda UKAWA wakionyesha furaha yao kwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Mgombea Urais wa Zanzibar katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad wakati alipowasili kwenye viwanja vya Jangwani Jijini Dar es salaam, kulikofanyika Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho, leo Agosti 29, 2015.
Sehemu ya Wanahabari kutoka Vyombo mbali mbali nchini wakiendelea kuchukua habari za Mkutano huo, uliofanyika jioni ya leo kwenye viwanja vya Jangwani Jijini Dar es salaam na kuhudhulia na maelfu ya Wakazi wa jiji hilo.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe akimkabidhi, Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa pamoja na Mgombea mwenza, Mh. Juma Duni Haji, Kitabu cha Ilani ya Uchaguzi ya Chama hicho kwa mwaka 2015/2020 mara baada ya kuizindua, leo Agosti 29, 2015.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, Mgombea mwenza, Mh. Juma Duni Haji pamoja na Mgombea Urais wa Zanzibar katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad wakionyesha vitabu cha Ilani ya Uchaguzi mara baada ya kuzinduliwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe.
Viongozi wa Vyama mbali mbali vinavyounda UKAWA wakionyesha Ilani hiyo mbele ya maelfu ya wakazi wa Jiji la Dar es salaam, leo Agosti 29, 2015.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe (kulia) akiwatambulisha baadhi ya Wagombea Ubunge katika Majimbo mbali mbali ya jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA, Mh. James Mbatia akizungumza kwenye Mkutano huo.
Watu wa Msalaba Mwekundu wakiwa wamembeba mmoja wa wakazi wa Jiji la Dar aliepoteza fahamu kwa kukosa hewa kutokana na uwingi wa watu uliofurika kwenye viwanja vya Jangwani, Jijini Dar es salaam leo Agosti 29, 2015.
Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Fredrick Sumaye akitoa salamu zake kwa wakazi wa Jiji la Dar es salaam waliofurika kwenye viwanja vya Jangwani jijini Dar es salaam leo Agosti 29, 2015.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akiteta jambo na Mgombea Mwenza wake, Mh. Juma Duni Haji, wakati wa Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho, uliofanyika leo Agosti 29, 2015. 
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akihutubia katika Mkutano huo wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho, uliofanyika leo Agosti 29, 2015.

Mmoja wa wanasiasa wakongwe waliotoka CCM, Tambwe Hiza akisalimia.









Wafuasi na wapenzi wa vyama vinavyounda UKAWA, wakifuatilia uzinduzi wa kampeni za Umoja huo katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam
.(Picha na Salmin Said)

Na: Hassan Hamad, OMKR.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mhe. Edward Lowassa amezitaja sekta za elimu, afya na kilimo kuwa ni miongoni mwa vipaumbele vyake kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.

Amesma sekta hizo ni muhimu kwa maendeleo ya wananchi ambapo amesema sekta ya kilimo itasaidia kuongeza ajira kwa vijana wanaokabiliwa na tatizo hilo kwa muda mrefu sasa.

Mhe. Lowassa ametaja vipaumbele hivyo katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam, kwenye mkutano wa hadhara wa uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho unaovijumuisha pia vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).

Kuhusu sekta ya afya amesema iwapo atachaguliwa kuongoza nchi anaimarisha huduma za afya ili kuhakikisha kuwa hospitali zote nchini zinapatiwa vitendelea kazi vya kutosha yakiwemo madawa, sambamba na kuimarisha huduma za akina mama na watoto.

Vipaumbele vyengine ambavyo ni sehemu ya Ilani ya uchaguzi ya Chadema amesema ni miundombinu na mawasiliano ambapo amewambia wafuasi wa UKAWA na wananchi kuwa ataijenga upya reli ya kati, ili kurahisisha mawasiliano katika eneo hilo.

Mapema akizindua Ilani ya Uchaguzi ya CHADEMA, Mwenyekiti wa Chama hicho Freeman Mbowe, amesema mabadiliko yanayopiganiwa na UKAWA yana lengo la kuleta maisha mapya kwa Watanzania, ikiwa ni pamoja na kuheshimu haki za binadamu.

Amesema Ilani hiyo ambayo ndio dira kwa vyama vyote vinavyounda Umoja wa UKAWA, imezingatia maslahi mapana ya Watanzania katika mazingira yaliyowazunguka.

Naye Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Frederick Sumaye amasema ameamua kujiunga na kambi ya upinzani ili kusaidia harakati za mabadiliko zinazopiganiwa na UKAWA.

Amesema Tanzania bado haijawahi kushuhudia mabadiliko ya kisiasa ndani ya mfumo wa vyama vingi, na kwamba UKAWA imejipanga vyema kuongoza mabadiliko katika uchaguzi mkuu ujao.

Aidha Mhe. Sumaye amemtaja Mhe. Lowasa kuwa ni mtu makini anayeweza kuongoza harakati za mabadiliko na kiongozi anayeweza kupambana na umaskiti unaowakabili wananchi.

Kwa upande wake mgombea mwenza wa Urais kupitia CHADEMA Mhe. Juma Duni Haji, amesema Chama hicho kinapigania mabadiliko ili kuondosha uonevu dhidi ya wananchi hasa wa kipato cha chini.

Ameidha ameahidi kutunza heshima za akina mama kwa kuimarisha huduma zao katika hospitali, ili kupunguza vifo vya akina mama wakati wa kujifungua ambavyo vimekuwa vikiathiri maendeleo na ustawi wa wananchi.

/ZanziNews

No comments :

Post a Comment