by makame silima
Ni vema viongozi wa UKAWA wakaelewa kuwa karibu vituo vyote vya kuandikisha wapiga kura kuna majina zaidi ya 200 kila kituo yameachwa na wahusika hawatambuliki na mfumo wa BVR na hivyo hawataruhusiwa kupiga kura.Mfano hai ni mimi mwenyewe ninaye post hili bandiko kwani nilijiandikisha na nina kitambulisho cha kupigia kura lakini nilipokwenda kwa ajili ya uhakiki nimekuta jina langu halipo na nilipoingia katika mitandao yote kuhakiki yaani kwenye simu na kwenye mtandao wa tume majibu ni kuwa sijajiandikisha na uhakiki ulipofanyika kupitia mashine ya BVR majibu ni no record.
Kwa hiyo kwa hiki kilichofanyika kimefanyika makusudi kwani hata hao wasimamizi waliopo katika vituo hivyo vya uhakiki hawana majibu jinsi ya kutatua tatizo hilo majibu yao ni kuwa hawana cha kufanya.
Maoni / Mapendekezo yangu.
UKAWA utoe agizo kwa viongozi wake wote katika majimbo yote nchini yaani visiwani na Bara watoe matangazo katika majimbo yao na wale wote wenye mapenzi mema na UKAWA ambao wana shahada na taarifa zao hazipo kwenye mfumo wa BVR wa Tume wajulikane na number za shahada zao ziorodheshwe na kujulikana wazi na viongozi husika walishughulikie suala hili kwa kupeleka malalamiko haya tume ili ufumbuzi upatikane kabla ya upigaji kura kwani hawa wahusika katika vituo huku mikoani hawana njia yeyote ya kutatua.
Viongozi wa UKAWA naombeni sana tena sana shughulikieni tatizo hili bila kufanya hivyo bao la mkono litatimia kwani kwenye ngome zote za CCM hakuna matatizo hayo isipokuwa ni kule kwenye maeneo ambayo CCM imekataliwa.
No comments :
Post a Comment