Alisema amegundua kuwa nchi haisongi mbele kwa sababu kuna viongozi wamepewa madaraka, lakini wamekuwa na kigugumizi kuchukua maamuzi magumu
Amesema yeye na safu yake atakayoiunda atakapoingia madarakani hawatakuwa na kigugumizi unapokuja wakati wa kuchukua maamuzi magumu na yenye maslahi kwa wananchi na taifa.
Aliyasema hayo kwa nyakati tofauti kwenye Jimbo la Bumbuli, mkoani Tanga na Bunda, mkoani Mara, wakati wa mwendelezo wa ziara zake za kampeni, ambapo jana alianza mkoani hapa.
Alisema amegundua kuwa nchi haisongi mbele kwa sababu kuna viongozi wamepewa madaraka, lakini wamekuwa na kigugumizi kuchukua maamuzi magumu na kwa wakati jambo aliloahidi kulivalia njuga iwapo Watanzania watampa ridhaa ya kuwa Rais.
Alitoa mfano kuwa, inashangaza kuona wanafunzi wengi wakikaa chini wakati nchi imejaaa misitu ambayo inaweza kutumika kutengeneza madawati. “Hili la kushindwa kuchukua maamuzi magumu na kwa wakati ndiyo limetufikisha hapa, hivi kunasababu ya watoto wetu kukaa chini na tuna misitu ya kutosha!....unakuta waziri wa maliasili yupo lakini tatizo ni maamuzi tu ...mimi sitavumilia hayo na waziri atakayekuwa legelege nitamwambia anipishe,” alisema Dk. Magufuli huku akishangiliwa na wananchi waliokuwa wakimsikiliza.
Aidha, alisema inashangaza kuona Watanzania wakiishi kwenye lindi la umaskini wakati nchi imejaa rasilimali za kutosha kama misitu, mito bahari, maziwa na wanyama na kwamba kinachokosekana ni maamuzi magumu na ya wakati.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment