dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, September 8, 2015

Lowassa asema atapunguza mshahara wa Rais toka milioni 400 kwa mwaka hadi milioni 24 kwa mwaka!




Katika hotuba yake amesema haingii ikulu kutafuta fedha anaenda ikulu kwa kazi moja tu ya kuhakikisha wananchi wanakuwa na maendeleo . Amesema dhamira yake ni kuona taifa linasonga mbele kwa kasi ya ajabu.
Amesema atapunguza mshahara wa Rais ambao analipwa hivi sasa dola 192,000 sawa na milioni mia nne kwa mwaka hadi kufikia milioni mbili kwa mwezi amesema kuna faida gani ya mtu kupokea mshahara wote huo ili hali wananchi wako hawana maji , zahanati hakuna dawa, pembejeo za kilimo zipo juu, wakulima wanakopwa mazao yao.

Amesema haendi ikulu kutafuta ela amesema anaenda ikulu kwa kazi moja tu ya kuondoa umaskini nchini hiyo ndiyo dhamira yake.

Amewashangaa wanaosema anafuata fedha ikulu na kuwaambia kama mtu umeshindwa kutafuta fedha ujanani halafu utegemee upate fedha uzeeni hiyo ni ngumu kwa sababu uzeeni ni muda wa kusaidia jamii kwa kile ulichochuma ujanani.

Amesema wakati wa mabadiliko ni sasa, na mabadiliko hayo yatapatikana nje ya CCM kwani ipo haja ya kubadilisha mfumo hodhi wa chama tawala kama kweli tunataka kusonga mbele sisi kama taifa. Amesema yapo baadhi ya mambo CCM hawawezi kuyabadilisha kwa kuhofia watu watafumbuka macho hivyo itatishia uhai wao
.
Source:Kengeteblog

No comments :

Post a Comment