- Akiwahutubia wakazi wa Turiani mkoani Morogoro leo, amesema katika Serikali yake atahakikisha anadhibiti ukosefu wa dawa katika vituo vya afya na hospitali ili kuhakikisha wananchi hawaendelei tena kuandikiwa vyeti na kwenda kununua katika maduka ya dawa.
Akiwahutubia wakazi wa Turiani mkoani Morogoro leo, amesema katika Serikali yake atahakikisha anadhibiti ukosefu wa dawa katika vituo vya afya na hospitali ili kuhakikisha wananchi hawaendelei tena kuandikiwa vyeti na kwenda kununua katika maduka ya dawa.
Hii ni mara ya kwanza kwa Dk Magufuli kugusia moja kwa moja mipango yake ya kudhibiti uharibifu wa dawa ambao huripotiwa kufanyika katika Bohari ya Dawa (MSD) yenye dhamana ya usambazaji dawa nchini.
"Tutaboresha masilahi ya manesi pamoja na madaktari ili waipende kazi na kuifanya kwa moyo, wale wanaotoka na madawa kule Dar es Salaam saa nyingine yanakaa mpaka yanaharibika bila kupelekwa yanakotakiwa. Hao mniachie nitalala nao mbele," alisema Dk Magufuli na kushangiliwa.
Ahadi hiyo hivi leo imeonekana kuwa kete ya ziada ya uboreshaji wa huduma za Afya nchini ambapo aliirudia tena katika mkutano wa Songe wilayani Kilindi.
"Lazima dawa zipatikane hospitali na huyo anayeleta dawa anakaa Dar es Salaam akae 'standby' (akae chonjo) kweli kweli, " alisema.
Mbali na kuhakikisha dawa zinapatikana wakati wote, mgombea huyo amesema Serikali itapeleka vitanda vya kutosha na kuhakikisha kila kijiji kina kituo cha afya na kila wilaya ina hospitali.
"Mimi siyo Shehe, siyo padri lakini nchi hii naifahamu vizuri tusibaguane hata kidogo. Tukibaguana, tutaanza dini kwa dini, kabila kwa kabila hata Wapare hapa wakaanza kuondolewa, hatutafika, " alisisitiza Dk Magufuli.
No comments :
Post a Comment