Maalim Seif alitoa kauli hiyo jana wakati wa mkutano wake wa kampeni za urais na kunadi sera za chama hicho katika viwanja vya Tibirinzi, Chake Chake, Pemba.
Aidha, alisema akichaguliwa ataunda utawala unaojali uhuru wa nchi, haki za kila Mzanzibari na maridhiano ya Wazanzibari.
Alisema vitendo vya rushwa na ufisadi vinadidimiza uchumi na maendeleo ya wananchi na kwamba hatokubali kuona vitendo hivyo vinaendelea na ataimarisha maslahi ya wafanyakazi wa serikali pamoja na kuwalipa stahiki zao.
Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, aliongeza kuwa lengo la serikali yake ni kuwaunganisha Wazanzibari na kuwapatia haki zao bila ubaguzi wa aina yoyote ili wajisikie kuwa uhuru ndani ya nchi yao.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment