Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, September 1, 2015

Magufuli aonya mabadiliko ya jazba.

Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli.
Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, amewaasa vijana nchini kuepuka kutaka mabadiliko kwa jazba.
 
Alitoa tahadhari hiyo jana katika kampeni za kujinadi na kuwanadi wagombea ubunge na udiwani wa chama hicho katika majimbo yaliyopo  wilayani Mbinga, Mkoa wa Ruvuma.
 
Magufuli alisisitiza kuwa vijana nchini hawapaswi kutaka mabadiliko kwa kutumia jazba kwa kuwa maendeleo yana changamoto zake.
 
Alisema hawawezi kukamilisha mambo yote kwa wakati mmoja na kutoa mfano wa Mungu kuwa hakuumba dunia kwa siku moja bali kwa siku sita.
 
Awali, aliahidi kujenga kwa kiwango cha lami barabara ya Mbinga hadi Mbambabay yenye urefu wa kilomita 66  kwa fedha za Benki ya Maendeleo ya Afrika.
 
Alisema upembuzi yakinifu na michoro imekamilika na kwamba barabara hiyo itaanza kujengwa mwezi ujao.
 
UMEME
Kuhusu matatizo ya ukosefu wa umeme wa uhakika yanayoukabili Mkoa wa Ruvuma, alisema serikali itakabiliana nayo kwa kuunganisha umeme wa Gridi ya Taifa mwezi ujao na kuachana na umeme wa jeneretaDk. Magufuli pia alisema anatambua kilimo cha kahawa kinachofanywa na Wana-Mbinga na atahakikisha wawekezaji wa ndani wanawezeshwa kujenga viwanda vya kisasa vya kahawa.
Alisema viwanda vikubwa, vya kati na vidogo vitawezesha vijana na wananchi wengine kupata ajira na kukuza uchumi wa mtu mmmoja.mmoja na Taifa kwa ujumla.
 
Alisema kila mkoa kitajengwa kiwanda kikubwa, na vyote vitakavyojengwa nchini vitasaidia kuchangia uchumi kwa asilimia 40.
 
Mgombea huyo alisema pia barabara ya Lituhi itaunganishwa na barabara kuu ya Songea na itakuwa ya kiwango cha lami, pia ataleta meli mpya katika Ziwa Nyasa na ujenzi wa barabara za mjini na majiji kwa kutumia fedha za Mfuko wa Barabara.
 
NYASA 
Akiwa wilayani Nyasa, aliahidi kujenga kiwanda cha kusindika samaki na daraja la mto Ruhulu ili kuondokana na matumizi ya kivuko chenye uwezo wa kuvusha magari manne kwa wakati mmoja kwenda upande wa pili.
 
Alisema pia serikali yake itajenga skimu ya umwagiliaji ili kuwezesha wananchi kuendesha kilimo cha umwagiliaji, hivyo kuwa na uhakikika sambamba na pembejeo za kilimo na wakulima kuuza mazao yao na kulipwa kwa wakati.
 
Aidha mgombea huyo aliahidi kujenga kwa kiwango cha lami barabara ya Mbinga hadi Nyasa na Nyasa hadi Ludewa, na kwamba yote yatawezekana kwa kuwa serikali yake itafanyakazi usiku na mchana.
 
VIWANJA VYA MAJIMAJI
Awali alipowasili kwenye Uwanja vya Majimaji Manispaa ya Songea jana, Magufuli alilakiwa na umati uliofurika hadi nje ya viwanja hiyo.
 
Mjumbe wa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) ya CCM, Dk. Emmanuel Nchimbi, alikuwa wa kwanza kumnadi kwa wananchi kwa kuomba kura za Dk. Magufuli.
 
 Nchimbi aliwaeleza wananchi kuwa yeye ni mkweli na anawahakikishia kuwa mgombea huyo anatosha.
 
“Sijawahi kuwadanganya angekuwa hana uwezo nisingepanda jukwaani kumuombea kura, tunatafuta rais na siyo mfano wa rais...Dk. Magufuli ni kiongozi bora na mwadilifu anatufaa kuwa rais,” Dk. Nchimbi. 
 
Nchimbi aliendelea kumnadi Magufuli akisema rekodi za Magufuli zipo tangu akiwa Wizara ya Ujenzi zikithibitisha kuwa akianzisha jambo anatekeleza na kuwatoa wasiwasi wananchi kuwa ahadi atakazotoa atazitekeleza watakapomchagua kuwa rais wa serikali ya awamu ya tano.
 
AJITAPA KUFUKUZA MAKANDARASI
Akijinadi kwa wananchi, Magufuli lisema alipokuwa Waziri wa Ujenzi alifukuza makandarasi 332 kwa uzembe.
 
“Kupambana na mafisadi siyo kazi rahisi, nimepambana nao nilivyokiwa Waziri, sikuchukua hata senti moja ya kandarasi kama yupo niliyechukua hela zake ajitokeze, wote niliowafukuza walijitakia, nina uzoefu wa kupambana na mafisadi, nipeni serikali ya awamu ya tano,” alisema.
 
 “Idadi hiyo ya makandarasi niliowafukuza kazi si ndogo na kumbukeni watu hawa ni wenye fedha nyingi, lakini kwa Magufuli waliweza kwenda kwa hiyo mkinipa ridhaa mafisadi kwangu hawatakatisha,” alisema.
 
Aidha, alitoa ahadi ya kuanza kutoa pensheni kwa wazee wote nchini kuanzia mwakani, kwa kuwa wazee hao walitoa mchango mkubwa kwa Taifa wakati wakiwa na nguvu zao kwenye shughuli mbalimbali walizokuwa wakizifanya.
 
RELI
Dk. Magufuli alisema tayari serikali iko mbioni kujenga reli kutoka Mtwara - Songea hadi Mbamba Bay, ili itumike kwenye shughuli za usafirishaji wa bidhaa mbalimbali katika maeneo hayo yakiwamo madini yaliyogundulika katika maeneo ya Mchuchuma na Liganga.
 
Aidha alisema reli hiyo itasaidia pia shughuli mbalimbali za kiuchumi kama za kibiashara kwa wananchi wa maeneo hayo.
 
VIWANDA
Dk. Magufuli alisema Tanzania atakayoiongoza yeye ni ya viwanda na kwa hali hiyo kama ilivyo kwa mikoa mingine, serikali yake itajenga viwanda mkoani Ruvuma kwa lengo la kutatua tatizo la ajira nchini
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment