Akizungumza na Nipashe jana jijini Dar es Salaam Ofisa wa Tume, Athumani Masesa, alisema uamuzi huo umetolewa baada ya kusikiliza rufaa 40 kati ya 56 zilizowekewa pingamizi. Makamba na Filikunjombe ni miongoni mwa wagombea waliotarajiwa kupita bila kupingwa baada ya kuwawekea pingamizi wapinzani wao, hasa kutoka vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Alisema tume hiyo ilitulipia mbali pingamizi nyingine 27 baada ya kupitia maelezo na kubaini kuwa hazikuwa na hoja za msingi za kuishawishi .
Aliyataja majimbo mengine kuwa ni Bumbuli ambalo mgombea wake wa CCM, January Makamba, Peramiho la mgombea wa chama hicho, Jenister Mhagama na Ludewa la Deo Filikunjombe.
Alisema Nec leo inatarajia kuendelea kupitia rufaa nyingine zilizobakia na baada ya kukamilisha kazi hiyo, wataanza kupitia 196 za madiwani kwa ajili ya maamuzi.
Awali waliotangazwa kupita bila kupingwa ni Makamba, Rashid Shangazi, Abdallah Chikota(Nanyamba) na Filikunjombe.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment