dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, September 9, 2015

Mkuu wa Wilaya ya Micheweni afariki, azikwa

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd; naye aliiungana na wananchi kisiwani Pemba katika mazishi ya Mkuu wa Wilaya ya Micheweni, Jabu Khamisi.


By Hassan Ali, Mwananchi.
Zanzibar. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, jana aliungana na wananchi kisiwani Pemba, katika mazishi ya Mkuu wa Wilaya ya Micheweni, Jabu Khamis Mbwana aliyefariki dunia jana kijijini kwake Kiuyu Micheweni.
Marehemu alizikwa mchana, kijijini hapo Micheweni na viongozi mbalimbali wa Serikali na wananchi walihudhuria mazishi hayo.
Akitoa salamu za Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, Balozi Seif alisema Dk Shein, amepokea kwa masikitiko msiba huo na kuwataka wananchi, wafiwa na familia ya marehemu kuwa wastahamilivu katika kipindi kigumu cha maombolezo.
Balozi Seif alisema Serikali ya Zanzibar, iko pamoja na familia ya marehemu na wananchi wa Wilaya ya Micheweni, katika kipindi hicho, kwani Mwenyezi Mungu ndiye mpangaji wa kila jambo.
“Muda huu nimepata taarifa kutoka kwa Rais anasema yuko pamoja na nyinyi wananchi wa Micheweni na kuwataka muwe na subira katika msiba huu”, alisema Balozi Seif.
Akitoa pole na kukabidhi ubani wake, Balozi Seif aliwataka familia ya marehemu, kuwa wastahamilivu, wavumilivu na wenyesubira katika kipindi hicho cha msiba.

No comments :

Post a Comment