Mgombea huyo aliwataka wananchi kumchagua na kuachana na mgombea huyo wa CCM ambaye
Akizindua mikutano ya kampeni zake katika jimbo hilo juzi, Chiragwire alitoa ahadi zaidi ya 10 ambazo alisema atazitekeleza iwapo atachaguliwa kuwa Mbunge kwa miaka mitano ijayo.
Mgombea huyo aliwataka wananchi kumchagua na kuachana na mgombea huyo wa CCM ambaye alijiuzulu nafasi ya Waziri wa Nishati na Madini kutokana na kashfa ya Akaunti ya Tegeta Escrow.
Akizungumza katika kijiji cha Mgango, kata ya Mgango, Jimbo la Musoma Vijijini, Chiragwire aliwataka wananchi kutorudia kufanya makosa katika kuchagua viongozi watakaowatekelezea ahadi zao.
Alisema wabunge waliowahi kuchaguliwa katika jimbo hilo walikuwa wakiahidi wananchi ahadi zisizotekelezeka na kuwatekeleza bila ya kupelekewa miradi ya maendeleo.Chiragwire aliahidi ahadi akichaguliwa kuwa Mbunge wa jimbo hilo, atahakikisha inajengwa barabara ya lami kutoka Musoma Mjini hadi Musoma Vijijini kupitia kijiji cha Busekera, ahadi ambayo iliwahi kutolewa na Rais Jakaya Kikwete, wakati akifanya kampeni zake za urais awamu yake ya kwanza 2005 na pili 2010, lakini haijatekelezwa.
Mgombea huyo alisema hata mgombea wa mwaka huu wa urais wa CCM, Dk. John Magufuli, akiwa waziri wa ujenzi na miundombinu aliwaahidi wananchi wa jimbo hilo kuweka lami barabara hiyo ili kurahisisha usafiri lakini mpaka sasa hajatekeleza.
Ahadi nyingine alizotoa ni kuhakikisha vijiji vyote vinapata maji safi na salama ya bomba, kuwapo na hospitali ya wilaya ili kupunguza umbali wa kufuata huduma Musoma Mjini na kinamama wajawazito, watoto chini ya miaka mitano na wazee kupata matibabu bure bila kulazimishwa wawe na kadi za bima ya matibabu.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment