Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, September 3, 2015

‘’Nassra mtoto aliekatisha ndoto za kusoma anaehitaji kusaidiwa’’

Written by hamed mazrui 


Ni Nassra Salum Khalid mkaazi wa Kilima hewa wilaya ya magharib Unguja ni mwanafunzi aliekatisha masomo yake ya darasa la saba siku chache kabla ya kukaribia kufanya mtihani wa Taifa kuingia kidato cha kwanza.

Nassra ni mtoto mwenye umri wa miaka kumi na tano anaesumbuliwa na maradhi ya mguu kwa muda wa miaka 14 sasa tokea akiwa na umri wa miezi 9 baada ya kuzaliwa na Mama yake mzazi Bi Mwamvua Ayubu Khamis .

Mzee Salum khamis Baba yake Nassra ni marehemu amefariki wakati mwanawe Nassra akiwa na miaka mitano tayari anasumbuliwa na maradhi haya ya mguu.

Mama yake Nassra anasema mwanawe alipata matatizo haya akiwa na umri wa miezi 9 wakati alipokwenda hospitali ya Mnazi mmoja Unguja kwa ajili ya kupiga sindano ya PPF ndio iliokuwa sababu ya matatizo haya yanayomtesa mtoto wake mpaka leo hii.

Mama wa Nassra ni mtu mwenye ucheshi na uchangamfu lakini ni mtu mwenye kuishi maisha duni yanayohitaji kusaidiwa katika kuhakikisha mwanawe anapata matibabu.

Mama huyu mjane kwa kiasi kikubwa amejitahidi sana kuhakikisha anafanikisha hili kutokana na uzito na uchungu wa mtoto wake zaidi anapoona wenzake wanakwenda skuli lakini mtoto wake ameshindwa kuendelea na skuli licha ya awali aliweza kwenda kwa kutumia magongo.

Katika jitihada za kutafuta matibabu ni mara tatu Nassra amefrikishwa hospitali India kwa msaada wa Serikali mara ya mwisho walitakiwa kurudi tena miezi mitatu baadae kutokana na mtoto wake kuwekewa kitu ambacho hawezi kukijua nikitu gani lakini anachokijua yeye nikuwa kitu hicho kinahitaji kutolewa na ndio maana wametakiwa kurudi tena India kwa matibabu zaidi lakini wameshindwa kufanya hivo kutokana na ukosefu wa fedha miezi sita sasa licha ya ahadi ya miezi mitatu waliotakiwa kurudi tena.

Kwa sasa hali ya Nassra inazidi kuwa mbaya mguu wake wenye uvimbe mkubwa sasa unatoka taka(usaha)kila wakati jambo ambalo linaiwia vigumu familia ya mama huyu mjane anaehitaji kusaidiwa.

‘’Nimekopa kuhakikisha Napata alau visa yangu na mwanagu ili niharakishe matibabu lakini kwa bahati naya nimeshindwa kutokana na umaskini wangu ma alisema Mama Nassra huku machozi yakimlenha’’
Gharama za matibabu wakati wanapelekwa na Serikali mara ya mwisho ilikuwa Dola alfu tano lakini kwa sasa inaweza kupanda kutokana na gharama kuongezeka.

Naomba kuchukua nafasi hii kupitia makala hii kuwaomba viongozi wote wa Serikali,wasiokuwa waserikali,watu binafsi kujitokeza kumsaidia mtoto huyu anaeteseka usiku na mchana kwa maumivu makali.

Wale wote wenye moyo wa kusaidia wanaweza kuwasilina na Mama mzazi kupitia nambari za simu 0776266380 au wanaweza kuwasiliana na mimi kwa maelekezo zaidi kupitia nambari hii 0774848800 au moja kwa moja swahiba fm redio mbweni Zanzibar.


No comments :

Post a Comment