Waziri Mkuu wa zamani wa serikali ya awamu ya tatu, Frederick Sumaye (Kushoto), mgombea ubunge wa Jimbo la Bumbuli kupitia CCM, January Makamba (Kulia)
Soni: Waziri Mkuu wa zamani wa serikali ya awamu ya tatu, Frederick Sumaye amemsifu mgombea ubunge wa Jimbo la Bumbuli kupitia CCM, January Makamba na kusema kuwa haelewi kwa nini anaendelea kungang’nia CCM wakati yeye si fisadi.
“January wewe si mwizi, kwa nini unang’ang’ania chama hicho,” alisema Sumaye wakati akizungumza katika mkutano wa kampeni kumnadi mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa, katika jimbo la Bumbuli jana.
Sumaye alikuwa akiwaambia wananchi wamuulize mbunge wao (January) kuhusu suala la wizi wa pembe za ndovu zilizokamatwa Hong Kong na madeni makubwa ya taifa kwa sababu anaweza kuwapa majibu kwasababu yeye ni msafi.
Katika mkutano huo, waziri mkuu huyo wa zamani alimtaka mgombea huyo na watu wengine wanaotaka kuhama wasiogope kufanya hivyo.
Aliwataka wananchi wapime wenyewe kama wanaamini kuwa CCM imetekeleza walioahidi basi wakichague na kama hakikutekeleza wafanye mabadiliko kama zilivyo nchi nyingine duniani.
Sumaye alisema kuwa CCM iliahidi maisha bora kwa kila Mtanzania lakini kimeshindwa kuetekeleza yale ambayo wamehidi hivyo Watanzania wanapaswa kukiweka kando na kufanya mabadiliko kama vile ilivyofanyika Kenya, Malawi na nchi nyingine walipoona vyama tawala havikuleta maendeleo.
No comments :
Post a Comment