dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, September 11, 2015

Tatizo la kifaa cha CT-Scan Muhimbili lishughulikiwe.

NA EDITOR

11th September 2015

Katuni.
Katika kipindi cha miaka mitano sasa, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili imekuwa ikikabiliwa na tatizo la ubovu wa mashine ya kipimo cha CT-Scan.
 
Kipimo hiki hutumika kupima mwili wa binadamu kubaini aina mbalimbali ya magonjwa yanayomsibu.
 
Hata hivyo, mara nyingi imekuwa ikiripotiwa kuhusu ubovu wa kifaa hiki na kuwafanya wagonjwa kulazimika kwenda katika hospitali binafsi kupata huduma.
 
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambayo ni kubwa kuliko zote nchini, kimsingi ni tegemeo la wananchi wengi kwa miaka mingi sasa.
 
Pamoja na jitihada kubwa za serikali katika kuboresha hospitali hiyo, lakini bado kuna maeneo ambayo yamekuwa na matatizo kwa miaka mingi sasa.
 
Katika kipindi cha kati ya miaka minne hadi mitano, imekuwa ikiripotiwa habari ya kuharibika kwa kipimo hicho cha CT-Scan katika Hospitali ya Taifa Muhimbili huku jitihada za kukabiliana na hali hiyo zikiwa ndogo. Kitendo cha kuharibika mara kwa mara kwa kifaa hicho kunazua maswali mengi na hasa kutokana na kuwaumiza wananchi ambao hulazimika kwenda kwenye hospitali nyingine kufuata huduma za CT-Scan na hivyo kuingia gharama kubwa.
 
Tunaishauri serikali kutilia mkazo suala hili kwa kuhakikisha matengenezo ya kifaa hiki muhimu katika hospitali hii kubwa ambayo ni kimbilio la Watanzania wengi kwa sasa.
 
Aidha, kutokana na kuharibika mara kwa mara kwa kifaa hicho, yapo mawazo kwamba sasa kuna umuhimu wa kununua CT-Scan nyingine kwa ajili ya hospitali hiyo.
 
Kwa mujibu wa uchunguzi tuliofanya, bei ya CT-Scan ni kati ya Dola 95,000 (sawa na Sh. milioni 201 ) na Dola 165,000 za Marekani (sawa na Sh. bilioni 3.5).
 
Ni dhahiri kwamba bei ya kifaa hicho ni kubwa, lakini tunaamini kuwa serikali ikipanga vipaumbele vyake sawasawa, basi ina uwezo wa kununua CT-Scan kwa ajili ya Hospitali ya Muhimbili kwani `kupanga ni kuchagua.’
 
Tunasema kwa hakika umefika wakati kwa viongozi wa serikali kulipa umuhimu suala hili ili kwa kuamua kununuliwa kwa CT-Scan ili kuwaondolea wagonjwa usumbufu wanaoupata.
 
Tunaamini serikali ikiamua inaweza kwani kifaa kimoja cha CT-Scan kinakaribiana kabisa na bei moja ya gari la aina ya Nissan Patrol, maarufu kama `mashangingi', yaliyotapakaa katika kila wizara, ofisi za serikali na hata halmashauri mbalimbali mikoani.
 
Kwa hakika tunajiuliza, kama uwezo wa kununua mashangingi lukuki tunao, tunashindwaje kununua CT-Scan?.
 
Achilia mbali fedha za kununua mashangingi, pia fedha zinazoelekezwa kwenye semina, warsha, makongamano, safari na shughuli zile kama vile za Siku ya Maji na nyingine ambazo zimekuwa zikigharimiwa kwa mamilioni ya fedha za serikali zinaweza zikaelekezwa kununulia kifaa hicho muhimu.
 
Ikumbukwe kwamba Taifa liko katika vita dhidi ya maadui watatu yaani ujinga, umaskini na maradhi.
 
Tunaiomba serikali ione umuhimu wa kufanya haraka kutengeneza mashine hiyo ya CT-Scan ama kuamua kununua nyingine mpya ili kuokoa maisha ya Watanzania wengi.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment