Juu ni Mhe Edward Lowassa ambae anatakiwa na Watanzania wanaoishi nje atoe uamuzi mgumu kuhusu uraia pacha kabla hajaapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!
- Watanzania wanaoishi ughaibuni wamkumbusha Mhe Lowassa juu ya kero yao!
“Mheshimiwa, tulikuletea barua yetu wiki 3 nyuma yakutaka ufafanuzi kama serikali yako itakubali kutupa Watanzania tunaoishi nje uraia pacha, yaani uraia wa nchi mbili, lakini mpaka leo hatujakusikia ukilizungumzia suala hili katika mkutano wako wowote ule – sio wewe wala sio mwenza wako Mhe Juma Duni Haji”.
“ Inawezekana kabisa kuwa labda barua yetu haikukufika japokuwa tuliileta kwa courier service kwa address ya Makao Makuu ya Chadema ya hapo mjini Dar Es Salaam. Kwahivyo, safari hii tumeona bora tukukumbushe kupitia njia hii ya blog”.
“Kila Mtanzania mwenye akili timamu tayari anajua na keshafahamu kwamba mambo ya tarehe 25 October, 2015 ni mambo ya kufuata taratibu za Katiba tu, lakini wewe tayari ushakuwa Rais wa nchi yetu na ndio maana tunakukumbusha ili tuje kusikia katika siku zako mia za mwanzo unatupa hizi habari nzuri kuhusu hili suala la uraia pacha”.
“ Mhe Lowassa, ikiwa picha zako tu kwenye mabango yaliyotundikwa mitaani mjini Dar Es Salaam zinaleta mafuriko ya watu, nani huyo ambae sio mwendawazimu atakaepinga kuwa wewe tayari sio Rais wa nchi hii? Hii ndio maana tunakukumbusha tena kwa mapema Mhe Lowassa kuwa tunachokitaka sisi ni uraia pacha wa kujivunia na sio kadi za kuishi Nyarugusu”.
“Kumbuka Mheshimwa kuwa, serikali tatu bila ya uraia pacha ni sawa na chai iliokosa mdalasini au hiliki”.
“Mwisho, tunakutakia wewe na timu yote ya Ukawa ushindi wa kishindo hio tarehe 25 October, ili wale wasiotutakia mema akina mzee Vijisenti na timu yake ya akina Prof Tiba iwe ndio mwisho wao kutuibia sisi wananchi maskini wa nchi hii”.
No comments :
Post a Comment