Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, September 3, 2015

WAFUASI WA DR.SLAA WA SHINYANGA MJINI WAHAMA CHADEMA!

Image result for breaking news

Katika
hali isiyokuwa ya kawaida vijana wengi wafuasi wa CHADEMA wa Shinyanga mjini wamechana kadi, bendera na flana za chama hicho kwa madai kimepoteza misingi yake na mwelekeo kwa kuwapokea mafisadi Lowassa na kundi lake.

Wakiwa na hasira baada ya kuisikiliza kwa kina hotuba ya Dr Slaa jana vijana hao wameandamana na kukusanyika katika ofisi za chama hicho wakimshutumu vikali mwenyekiti wao Taifa Freeman Mbowe kwa kukiuza chama kwa Fisadi lowasa na kusababisha kuwaengua viongozi wa juu wa chama hicho akiwemo Dr slaa, Mnyika na Lisu wakiwa kwenye benchi huku chama kikitwaliwa na mafisadi Lowassa, Sumaye, Masha na makapi yao.

"Wamesikika kwa hasira wakisema Mbowe kauza chama chetu, hatutokubali kamwe na hatutaruhusu hili, Mbowe asije kabisa shinyanga na lowasa wake, kwanza aturudishie chama chetu na pesa alizolipwa bilioni 50 azirudishe kwa Lowassa msaliti mkubwa huyo, anajifanya mzalendo, kamanda kumbe fisadi mkubwa ametuuza mchana kweupe.

Hapa Shinyanga CHADEMA na Mbowe anatuhumiwa kuleta mgombea ambaye sie mkazi/mwenyeji wa Shinyanga na hakubaliki kabisa na wakazi wa Shinyanga. Mgombea huyo Patrobasi Katambi amepora nafasi ya ndugu yetu Kasili ambaye ni mkazi wa Shinyanga.

"Sisi tutampigia kura Rais Magufuli na mbunge masele, wao wamemwaga mboga sisi tunamwaga ugali tulale njaaa wote.Bora CCM waendelee kutawala tu kuliko kudanganywa na chadema kama watoto. Imekula kwao.

CHANZO: JAMII FORUM

No comments :

Post a Comment