Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, October 1, 2015

AHADI: Dk. Magufuli - Wafugaji, wakulima wakipigana RCs, DCs nawafukuza.

Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli.
Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli (pichani), amesema wakuu wa mikoa na wilaya ambao maeneo yao yatakumbwa na mapigano ya wakulima na wafugaji akiwa madarakani atawafukuza kazi siku hiyo hiyo.
 
Aliyasema hayo jana kwenye mkutano wake wa kampeni katika Jimbo la Mpwapwa mkoani Dodoma, mkoa ambao mapigano ya wakulina na wafugaji yamekuwa sehemu ya maisha.
 
Alisema lazima mapigano ya wakulima na wafugaji yafike mwisho na kama kuna watendaji watazembea kuchukua hatua, basi yeye atawawajibisha haraka.
 
“Haiwezekani watu waendelee kuuana wakati viongozi wapo, mimi Magufuli, mkuu wa mkoa au wilaya ambaye eneo lake litakumbwa na mapigano, nitamfukuza kazi siku hiyo hiyo maana atakuwa ameshindwa kazi,” alisema.Alizipa pole familia zilizopoteza ndugu na jamaa kutokana na mapigano hayo na kuahidi kuwa akiingia madarakani atahakikisha hali hiyo haitokei kwa sababu atawabana viongozi wawajibike.
 
Akiwa katika Jimbo la Kongwa, Dk. Magufuli alisema serikali yake itawabana wawekezaji kutoka nje ili waajiri wafanyakazi wengi wa Kitanzania badala ya kuja na watu wao.
 
Alisema kuna Watanzania wengi ambao wamesoma na wana utaalam wa fani mbalimbali, hivyo hatakubali wawekezaji hao kuajiri wageni kwenye nafasi ambazo hata Watanzania wanazimudu.
 
Dk. Magufuli vile vile, alisema serikali yake itawahamasisha wanafunzi wanaomaliza vyuo vikuu kujiunga kwenye vikundi ili wakopeshwe mitaji ya kuanzisha viwanda na kampuni.
 
Alisema vijana hao watakopeshwa bila riba ili wazalishe bidhaa mbalimbali, hali itakayosababisha kuongezeka kwa nafasi nyingi za ajira.
 
Pia aliwaambia wakazi hao wa Kongwa na Kibaigwa kwamba serikali yake itahakikisha hakuna mwananchi anayekufa kwa njaa.
 
Alisema anakusudia kuwawekea mazingira mazuri wakulima wa Tanzania ili bidhaa wanazolima ziwe na bei nzuri, hali itakayowavutia wakulima wengi kulima kilimo cha kibiashara na kuondokana na umaskini.
 
 
Polisi wakanusha karatasi za kura kukamatwa Masasi.
 
Na Juma Mohamed, Mtwara
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara limekanusha taarifa zinazodaiwa kuandikwa katika mtandao mmoja wa kijamii, zikidai kukamatwa kwa baadhi ya watu katika kituo cha polisi wilaya ya Masasi mkoani hapa wakiwa na masanduku na fomu za kupigia kura zipatazo 2000 zikiwa tayari zimetumika.
 
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Henry Mwaibambe, alisema taarifa hizo zilidai kuwa, fomu hizo zilimpa alama ya vema mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli na mgombea ubunge wa jimbo la Masasi kupitia chama hicho.
 
 Alisema taarifa hiyo iliendelea kudai kuwa, mkuu wa wilaya ya Masasi aliingilia kati na watuhumiwa hao ambao hawakutajwa majina waliachiwa huru kwa dhamana kwa amri ya mkuu huyo wa wilaya ambaye ndiye aliewadhamini na kwamba masanduku hayo na karatasi yamehifadhiwa katika kituo cha polisi wilayani humo.
 
Kamanda Mwaibambe alisema taarifa hiyo ni uzushi na upotoshaji mkubwa na kwamba hakuna mtuhumiwa wala masanduku yaliyokamatwa mkoani hapa wala katika wilaya hiyo.
 
“Tunachofahamu kupitia kwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (Nec), vifaa vya kupigia kura bado havijawasili nchini na alituahidi vitaanza kuwasili mwishoni mwa mwezi huu kutoka nchini Afrika Kusini.” alisema.
 
Alisema Jeshi la Polisi linamsaka mhalifu huyo wa mtandaoni na akitiwa mbaroni atafikishwa katika vyombo vya sheria.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment