Kauli hiyo aliitoa jana kwenye uwanja wa Mnadani uliopo wilayani Sengerema mkoani Mwanza, kuwa akiingia madarakani atahakikisha vivuko vyote havitozi nauli ili kutoa unafuu kwa wananchi.
“Kama Kenya na nchi nyingine, vivuko ni bure, kwa nini sisi Tanzania tushindwe...nawahakikishia nikiingia madarakani vivuko vitakuwa bure,” alisema.
Aidha, alisema atahakikisha wakulima wote wanalima kilimo cha kisasa ikiwa ni pamoja na kufuta ushuru wa mazao ili waweze kuuza mazao yao ndani na nje ya nchi.
Alisema wakulima wanalima mazao mengi lakini wanapata shida kuuza mazao yao kwa sababu hawana masoko.
“Nitahakikisha wanauza mazao yao ndani na nje ya nchi, na siyo kulima mazao mengi halafu yanaozea ndani,” alisema.
MBOWE
Akizungumza kwenye mkutano huo, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alisema katika uongozi wa Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, mgombea wa CCM, Dk. John Magufuli, waliamua kugawana nyumba za serikali zilizojengwa kipindi cha Hayati Baba wa Taifa, Julius Nyerere.
Aliongeza kuwa Magufuli alitumia ofisi yake kuingia mikataba hewa na kutoa makandarasi walio chini ya kiwango na kujenga barabara ambazo hazina kiwango.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment