Mwenyekiti wa Chama Cha Democratic Party DP Mch. Christpher Mtikila amefariki alfajiri ya Leo katika ajali ya Gari iliyotokea Msolwa Bagamoyo.
0000
Mwanasiasa mkongwe na Mwenyekiti wa Chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila amefariki dunia leo alfajiri kwa ajali ya gari katika Kijiji cha Msolwa, Chalinze, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Jaffar Mohamed amethibitisha.
RPC Mohamed amesema Mtikila alikuwa akitokea Morogoro kuelekea Dar es Salaam na alikuw na watu wengine watatu katika gari hilo ambao wamejeruhiwa.
Amesema chanzo cha ajali hiyo bado kinachunguzwa. Taarifa zaidi zitakujia kadri tutakavyozipokea.
/Mwananchi.
No comments :
Post a Comment