Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Wazee wa Jimbo la Kojani alipowasili katika viwanja vya mpira kiungoni Wilaya ya Wete Pemba kwa kuaza Mkutano wake wa Kampeni kisiwani Pemba.
Kikundi cha Taraab cha Mzee Gogo Kangagani kikitoa burudani katika viwanja vya Mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, katika viwanja vya mpira kiungoni Wilaya ya Wete Pemba.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Wete Pemba Ndg Kombo Hamad Yussuf, akizungumza wakati wa mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein uliofanyika katika viwanja vya mpira kiungoni Pemba.
Wananchama wa CCM Jimbo la Kiungoni Pemba wakifuatilia Mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, uliofanyika katika viwanja hivyo.
Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dk Ali Mohamed Shein, akiwa na Viongozi wa CCM wakimsikiliza Mwenyekiti wa CCM Wilaya Wete wakiti akihutubia katika mkutano huo na kuwataka Wan anchi Kisiwani Pemba kumpigia Kura ya Ndio Dk Shein na Wagombea wote wa CCM.
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein, akimpokea aliyekuwa Mwanachama wa CUF Ndg Rashid Mohammed Hassan,kwa kuamua kujiunga na CCM, na kumkabidhi Kadi yake ya CUF Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Shein, wakati wa mkutano wake wa Kampeni uliofanyika katika viwanja vya kiungoni Wilaya ya Wete Pemba Jumla ya Wanachama wapya 38 wamejiunga na CCM wakitikea CUF.
No comments :
Post a Comment