Mwanachama wa CCM Jimbo la Mpendae akiwa amevaa fulana yenye ujumbe muhimu
Vijana wa Jimbo la Mpendae wakishangilia wakati wa mkutano wao wa Kampeni wa Jimbo hilo uliofanyika katika viwanja vya mpira bustani ya Migombani.
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mpendae Mhe Issa Kassim Issa akiwahutubia Wananchi wa Jimbo hilo wakati wa mkutano wa kampeni wa Wagombea Ubunge Uwakilishi na Udiwani uliofanyika katika viwanja vya bustani ya Migombani Unguja na kuwaombea kura kwa Wananchi wa Jimbo hilo.
Mwenyekiti wa Wilaya ya Amani CCM Ndg Abdi Ali Mzee akiwahutubia wananchi wa Jimbo la Mpendae wakati wa mkutano wa kampeni wa Jimbo hilo na kuwataka kukipigia kura ya Ndio Chama cha Mapinduzi na Wagombea wake wote.
Mgombea Uwakilishi Jimbo la Jangombe Zanzibar Ndg Abdalla Diwani, akiwasalimia Wananchi wa Jimbo la Mpendae wakati wa mkutano huo wa kampeni wa wagombea wa Jimbo la Mpendae uliofanyika katika viwanja vya bustani ya migombani Zanzibar.
Mgombea Uwakilishi Jimbo la Kiembesamaki Zanzibar Mhe Mahmoud Thabit Kombo, akiwasalimia Wananchi wa Jimbo la Mpendae wakati wa mkutano huo wa kampeni wa wagombea wa Jimbo la Mpendae uliofanyika katika viwanja vya bustani ya migombani Zanzibar.
Katibu Mwenezi wa Wilaya ya Amani Kichama Ndg Juma Resi akimtambulisha Mgombea Uwakilishi wa Jimbo la Mpendae Mhe Mohammed Dimwa, wakati wa mkutano wa kampeni wa jimbo hilo kuomba kura kwa Wananchi wa Jimbo hilo
Katibu Mwenezi wa Wilaya ya Amani Kichama Ndg Juma Resi akimtambulisha Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mpendae Mhe Salim Turky, wakati wa mkutano wa kampeni wa jimbo hilo kuomba kura kwa Wananchi wa Jimbo hilo
Mgombea Ubunge Jimbo la Mpendae Zanzibar Mhe Salim Turky akiwahutubia wananchi wa jimbo la mpendae wakati wa mkutano wa kameni uliofanyika viwanja vya bustani ya migombani na kuwaahidi vijana ajira katika jimbo hilo katika kiwanda cha kutengenezea vibiriti ambacho kitanjengwa katika jimbo hilo na kutoa ajira kwa vijana.
Taswira wakati wa mkutano wa kampeni ya Wagombea wa Jimbo la Mpendae Viwanja vya Bustanini Migombani Zanzibar.
/ZanziNews.
No comments :
Post a Comment