Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, October 1, 2015

Nec yakemea matusi na kejeli kampeni za vyama

Mwenyekiti wa Nec, Jaji mstaafu, Damian Lubuva
Ikiwa zimebaki siku 24 kuhitimishwa kwa kampeni za uchaguzi mkuu na kufanya uchaguzi Oktoba 25, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), imevishukia vyama vinavyoendesha kampeni zake kwa kujadili watu na kuingilia utendaji kazi wa kila siku wa Tume.
 
Licha ya kuwapo kwa vyama 23, mchuano mkali ni kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM)na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) unaoundwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Chama cha wananchi CUF, NLD na NCCR-Mageuzi ambavyo vimesimamisha mgombea mmoja na ambavyo vinaonekana kunyooshewa kidole na Tume.
 
Mwenyekiti wa Nec, Jaji mstaafu, Damian Lubuva, alitoa onyo hilo jijini Dar es Salaam jana wakati akifungua mkutano wa Tume na wawakilishi wa watu wenye ulemavu nchini.
 
Alisema tangu kuanza kwa kampeni za uchaguzi Agosti 22, mwaka huu, baadhi ya wagombea walizidisha muda na kuonywa na Tume, lakini kadiri siku zinavyosonga mbele, wanaishiwa sera na kuanza kutumia muda mrefu kuwasema watu na kuingilia utendaji kazi wa Tume.“Kuna vyama vimeishiwa sera na sasa wapambe wake wanatumia muda mwingi kutoa lugha zisizo za staha na kukashfu dhidi ya wagombea wengine. Vingine vinavuka mipaka yake na kuingilia utendaji kazi wa Tume. Tunawataka waeleze sera zao kwa wananchi kama wameishiwa watulie hadi siku ya kupiga kura,” alisema na kuongeza:
“Hatutaki kampeni za kuzungumzia watu, elezeni sera zenu kwa lugha inayopendeza, tumetoa onyo kali la mwisho na iwapo wataendelea, tutachukua hatua kwa kuwaita kwenye Kamati ya Maadili ya Tume.”
 
Aidha, alisema anavishangaa vyama ambavyo vinaacha kunadi sera na kuingilia majukumu ya Tume kwa kueleza kuna uhamisho wa watumishi ndani ya Tume, jambo ambalo wanajua wazi kuwa siyo kazi yao.
 
“Mambo ya utawala ya Tume tuachiwe wenyewe, hatuko tayari kuingiliwa na yeyote,” alisisitiza.
 
Jaji Lubuva alisema baadhi ya vyama vinadai kuwa kuna wizi wa kura na kuvitaka kueleza jinsi zinavyoibwa.
 
“Wewe siyo mpishi wa chakula, unaingiliaje kutaka kujua mpishi amebadilishwa au la, huko ni kufanya majukumu yasiyokuhusu. Subiri chakula kipikwe uletewe ule…wanadai kura zinaibwa, watueleze ni dirisha gani linatumika ili tuzibe kwa saruji na nondo,” alifafanua.
 
Alisema kuanzia sasa, Nec haitafumbia macho uvunjifu wowote wa kanuni na vyama vitakavyovuka mpaka, vitapelekwa kwenye kamati ya maadili na adhabu wanazoweza kupewa ni onyo kali au kufungiwa wasifanye kampeni.
 
“Fanyeni kampeni zenu kwa kuzingatia maadili mliyoyasaini, acheni kudodosa mambo yasiyowahusu,” alisema.
CCM ni moja ya chama ambacho wapambe wake wamepanda kwenye majukwaa ya kumuombea kura mgombea urais wao, Dk. John Magufuli, na kuanza kumshambulia mgombea wa Chadema kwa maneno yasiyo na staha.
 
Hivi karibuni, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, iliishutumu Nec kwa kufanya mabadiliko ya watumishi wake ikiwamo kuwapo kwa Maofisa wa Usalama wa Taifa wanaowatisha watumishi na wanajeshi kuingizwa kwenye Tume.
 
Mbowe alimtaja Naibu Katibu wa Tume na Mkurugenzi wa Tehama, Dk. Sisti Carih, amehamishwa baada ya kutolewa ofisini na kukaguliwa na Maofisa Usalama.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment